CHATANDA AWATAKA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KWENYE UCHAGUZI UJAO.

 


Na Francisco Peter.

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake (UWT) Taifa Merry Chatanda amewasisitiza wanawake kuhamasika kikamilifu katika uongozi ambapo changamoto inaonyesha uchache wa wanawake wanogombea katika nafasi mbalimbali.


Amesema kuelekea uchaguzi ni jukumu la kila mwanamke kushawishi kugombea katika nafasi mbalimbali, Serikali ya Awamu ya sita imekuwa ikichukua hatua kadhaa ili kuondoa vizingiti vinavyoweza kuwazuia wanawake kushiriki kikamilifu.


"Kwasasa jukumu nililonalo ni kuwashawishi wanawake kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani 2025" Amesema Chatanda.


Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu unaweka wazi demokrasia ambapo usawa wa kijinsia ni dhamira ya Chama kupata wagombea watakaofaa na kuputishwa katika nafasi mbalimbali.


Naye katibu wa CCM wilaya ya ilala Bi fratha katumwa Alisema kuelekea uchaguzi wao kama viongozi wamekuwa wakihamasisha mashina mbalimbali wanachama wao kujua umuhimu wa kupiga kura.


"Tumekuwa tukipita katika mashina kunadi ilani ya CCM huku tukikutana na wajumbe mbalimbali na kuwaeleza kuhamasisha wanachama kuweza kupita maeneo katika kuwafikia wanajamii kujua umuhimu huo wa kupiga kura " alisema Katumwa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.