TTCL KUTOA HUDUMA ZA MKONGO WA MAWASILIANO NCHINI BURUNDI NA BAADHI YA NCHI NYINGNE AFRIKA KWA GHARAMA NAFUU.
Na Emmanuel Kawau,
Dar Es Salaam.
Tanzania na Burundi zatiliana saini mkataba wa huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kwa kuunganisha Mkongo wa Tanzania kuweza kuhudumia Mkongo wa Burundi.
Mkataba huo umesainiwa Shirika la Mawasiliano (TTCL) Kwa upande wa Tanzania na kwa Burundi umesainiwa na BBS (Burundi Backbone system) huku ukiwa ni mkataba wa miaka mitano ukiwa na thamani ya Dola za Kimarekani milioni tatu nukta tau (3.3) sawa Shilingi za Kitanzania Bilioni Nane nukta tatu (8.3).
Akizungumza katika Hafla ya utiliaji Saini Makubaliano hayo kibiashara leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Mawasiliano na Tenknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa utiliaji sani kati ya TTCL na BBS Kutaongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi katika nyanja mbalimbali na kuongeza Soko la kibiashara."Serikali ya Awamu ya sita imelenga kukuza Sekta ya Mawasilino kwa kuimarisha Huduma za Mkongo wa Taifa ilikuweza kukuza Uchumi wa kidigitali"asema Waziri Nape
Aidha ametoa wito kwa nchi zote za Bara la Afrika kuweza kujiunga na Mkongo wa Mawasiliano wa Tanzania ili kupata huduma bora kwani mkongo huo umeendelea kuimarishwa siku hadi siku.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga amesema Shirika liko tayari kutoa huduma bora kwa Burundi kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa kibiashara. "Tunaamini ushirikiano huu utaimarisha uhusiano wa kindugu kati ya nchi zetu na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamiii kwa wananchi wa Tanzania na Burundi".
Ameongeza kuwa mapema mwaka jana 2023, shirika lilifanikiwa kusaini Mkataba wa kibiashara wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Tanzania na Mkongo wa Taifa wa Uganda kwa kushirikiana na Mamlaka ya Taifa ya Teknolojia ya Habari ya Uganda (NITA-U). Pia, 4 lilifanikiwa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Tanzania na Mkongo wa Taifa wa Malawi kupitia Shirika la Umeme la Malawi (ESCOM).
Ameongeza kuwa hadi sasa, wamefanikiwa kuunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, na Zambia. Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeishafika Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji, na juhudi za dhati zinaendelea za kuunganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utekelezaji wake unaendelea.
Shirika linaendelea kusimiamia ujenzi wa miradi ya upanuzi wa Mkongo wa Taifa kikamilifu na matarajio yao miradi hiyo itakamilika haraka.
Miradi hiyo pamoja na Awamu ya Kwanza yenye Km 4,442 ambayo itafikia wilaya 22, Awamu ya Pili yenye Km 1,520 ambayo itafikia wilaya 32 na Upanuzi wa Njia Kuu kutoka 800Gbps hadi 2Tbps kwa mizunguko ya Kaskazini na Magharibi; na Awamu ya Tatu yenye Km 928 ambayo itafikia Wilaya 5 vinajengwa pamoja na upanuzi wa hadi 2Tbps kwenye mradi wa upanuzi wa ndani kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa BBS Jeremy Kageringwe amesema kupitia mkataba huo mpya wliosaini hii leo unatoa fursa ya kuongeza kasi ya mtandao hivyo kuufanya kiwa na kasi mara dufu.
Pia amesema mkongo huo una manufaa ya kiuchumi na kibiashara baina ya Burundi na Tanzania kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili.


Hakuna maoni: