TAASISI YA MYLEGACY YAWASISITIZA VIJANA KUONA UMUHIMU WA KUJITOLEA KWA JAMII.


Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Vijana hususani wanaomaliza Vyuo wametakiwa kupendelea kujitolea kwenye taasisi mbalimbali huku wakingojea ajira ili kupata ujuzi unaohitajika kwenye sekta ya ajira Duniani.

Akizungumza katika mkutano kati ya Taasisi ya Urithi wangu (MyLegacy) na vijana waliochini ya mpango maalumu wa kujitolea Mratibu wa Program MyLegacy Amina Ally amesema vijana wengi wanaomaliza Vyuo wanakuwa hawana ujuzi unahitajika katika Ajira wanazozihitaji.


"Tunajua kwamba vijana wanapotoka chuo mara nyingi wanakuwa hawana ule ujuzi wanaouhitaji kwenda kujipatia ajira,kwahiyo tunawapokea na kufanya nao kazi ili hata watakapokuja kuondoka na kupata kazi sehemu nyingine basi wataweza kutumia ujuzi wanaoupata hapa". Amesema Bi Amina.


Aidha MyLegacy inafanyaka katika maeneo mbalimbali hususani kusaidia wanawake na vijana kiuchumi,maswala ya uongozi jumuishi na utetezi wa haki za wanawake na watoto.

"MyLegacy inafanyakazi na watoto pia hususani walioko shuleni kupitia vilabu, na ndani ya hivyo vilabu vya shule wanafanya shughuli mbalimbali za kujitolea,ikiwemo maswala ya usafi kujitolea kuhamasisha maswala ya uongozi lakini pia maswala ya hedhi salama na usafi wa hedhi, wanatengeneza sodo za kufua na wengine wanatengeneza sabuni na wengine wamepanda miti na bustani kuhakikisha wanaboresha mazingira" Amesema Bi Amina na kuongeza kuwa 

"Pia tunafanyakazi na walimu ambao wao sasa wanafanyakzi ya kusimamia vilabu mashuleni,kusimamia miradi ambayo ipo ndani ya hiyo shule"

Bi amina ameongeza kuwa ukiachana na kundi hilo pia wanafanyakazi na makundi mbalimbali ya kujitolea kwenye jamii ikiwemo green beach wanaofanyakazi ya kusafisha mazingira,wawaka kikundi cha watu wenye mahitaji maaalum wanaofanyakazi ya ujasiliamali kawe,ambao wamejikita kusaidia watu wenye ulemavu kupata elimu ya ujasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye mahitaji maalumu wawaka kawe Mlisho Bilali amesema MyLegacy imekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwa kutoa elimu mbalimbali na kuiwezesha jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali.

"Mimi nawashukuru MyLegacy wametujengea kujiamini,na kuweza kuifikia jamii kubwa ya wenye ulemavu kuweza kufanya jamboo na kukaa pamoja na kuweza kufanyakazi za ujasiliamali ambapo inaweza ikawa ngumu kwa watu wenye ulemavu kupata kazi ofisini lakini kupitia ujasiliamali tunaweza kupata kipato na kuendewha familia zetu"


Nae mmoja wa vijana anaoetekeleza program ya kujitolea Meshack Daniel ambaye anafanyakazi ya kujitolea na MyLegacy kama Afisa Mawasiliano ambapo amebainisha kuwa kujitolea kumsaidia kubadilisha mtazamo na kubaini kuwa kujitolea ni njia moja wapo ya kuitumikia jamii.


"Kupitia MyLegacy nikiweza kushirikiana na Team, team ya MyLegacy wengi wanafanyakazi katika taaluma tofauti kuanzia uongozi ,na MyLegacy ni moja ya taasisi ambayo inafanyika kazi katika viwango vya Kimataifa hivyo kunifanya kufanyakazi katika viwango tofauti na nawali na kunitofautisha na wengine na kunijengea kujiamini".

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.