WIZARA YA AFYA YATAHADHARISHA TIBA ZA KIENYEJI KWENYE UGONJWA WA MACHO MEKUNDU.


Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Wizara ya Afya imeitaka jamii kuacha tabia ya kutumia dawa kiholela ili kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa macho mekundu (Red Eyes).


Wito huo unakaja mara baada ya Wizara ya Afya kubaini Wagonjwa wanne wa macho mekundu kuwa na vidondo kwenye mboni ya jicho vilivyotokana na tiba isiyosahihi, ikiwemo kutumia maji chumvi,Chai,mchaichai,tangawizi na vitu vingine ambavyo hutumia kuweka kwenye macho na kuhatarisha afya.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya zilizopo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara hiyo Prof. Paschal Ruggajo ambapo amesema ugonjwa wa macho mekundu hausababishi upofu.


"Red Eyes hauleti upofu labda pale mtu anapozembea na kupata maambukizi ya pili,ama kutumia tiba zisizo sahihi ,tunasisitiza wagonjwa wasitumie dawa bila maelezo ya Daktari" Amesema Prof Ruggajo Nakusisitiza wa kusema

 "Maduka ya dawa tunayataka kuendelea kufuata miongozo ya ya Wizara ya Afya ambayo inawataka wasiuze dawa pasipo cheti cha Daktari".


Prof. Paschal amewataka wananchi endapo wataona dalili za maumivu makali kwenye macho kufika hospitalini haraka iwezekanavyo ili kupata madhara makubwa zaidi.


Aidha amewataka wale wote wanaotoa elimu kiholela katika Mitandao ya kijamii kuacha mara moja na kuwasisitiza wanajamii kupuuza taarifa zisizotoka kwenye vyanzo sahihi ambavyo ni Wizara ya afya, hospital, na vyombo vya habari.


"Tunawataka Wananchi wachukue tahadhari na wafike hospital kupata tiba sahihi. Ugonjwa wa macho mekundu hausababishi upofu lakini tiba zisizo rasmi zinaweza kupelekea kutokea kwa upofu" 


Mpaka sasa wagonjwa wa machi mekundu waliofika katika vituo vya afya wanaripotiwa kuwa zaidi ya 13,000 huku mikoa 23 ikiripotiwa kuwa na wagonjwa ambapo mikoa ya Dar es salaam na pwani inatajwa kuongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.