Na Mwandishi wetu, Ngorongoro - Arusha.
Hamasa ya kujiandikisha na kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni inazidi kupamba moto baada ya kundi la 5 la awamu ya pili kuhama likiwa na kaya 67 zenye watu 592 na Mifugo 2,790.
Wananchi hao waliokuwa wakiishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuamua kuhama kwa hiyari wameagwa rasmi siku ya Alhamisi 01.02.2024.
Kamishina wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw.Richard Kiiza ambapo aliwaomba wenyeji wanaohama kutumia fursa waliopata kuendelea kuwapa habari na kuwashawishi ndugu zao ambao bado hawajajiandikisha ili waweze kujiandikisha na kuondokana na maisha duni wanayoishi ndani ya Hifadhi.
Alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea na uhamasishaji wa wananchi ambapo kwa sasa mwamko wa watu wanaoishi ndani ya hifadhi kutaka kuondoka umeongezeka huku akisisitiza kuwa serikali itaendelea kuheshimu haki zote za msingi za wananchi hao.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mamlaka hiyo. Fedes Mdala ambaye pia ni Meneja wa mradi huo amesema kuwa hadi kufikia sasa jumla ya kaya 934 zenye watu 5,747 na mifugo 26,227 zimeshaondoka ndani ya hifadhi.
Mdalla amesema hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo zimeendelea kuchukuliwa na kuzitaja hatua hizo kuwa ni ujenzi wa nyumba, uhamasishaji, Uandikishaji wa maendeleo yaliyofanywa ndani ya Hifadhi na uhamishaji wa wanachi kwenda Msomera na maeneo mengine.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka wizara ya Mailiasili na Utalii John Mapepele amewapongeza wananchi hao kwa kufanya uamuzi sahihi ambao




Hakuna maoni: