TRA lMETAKIWA KUBAINI FEDHA ZINATOTENGWA NA MAKAMPUNI, TAASISI ZIWAFIKIE WATU WENYE MAHITAJI MAALUM.
DAR ES SALAAM:
Na Mariam Muhando
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo meitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuhakikisha wanapofunga hesabu zao za mwaka waangalie fedha zinazotengwa na Makampuni na Tasisi mbalimbali kwa ajili ya Watu wenye mahitaji maalum ili kubaini Watanzania wanaostahili kunufaika na fedha hizo ziwasaidie katika mahitaji yao.
Mkuu wa Wilaya hiyo ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya zoezi la kugawa vifaa vya Watu wenye mahitaji maalum Kwa Walimu na Wanafunzi lililofanyika kwenye shule ya Msingi Uhuru Wasichana iliopo Wilayani humo Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kuwasaidia katika utendaji kazi wao.Mpogolo amesema zoezi hilo ni la kihistoria halijawai kutokea katika utendaji kazi wake kwani tukio hilo ni moja kati ya matendo ya huruma Kwa Watu hao ambayo yanadhihirisha upendo kwenye kuwasaidia mahitaji yao. "Hivyo ninaishukuru Benki ya NMB Kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuisaidia jamii, Hivyo waendelee kuwasaidia Watu hao ikiwa bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali".
Pia ameendelea kuishukuru NMB Kwa kuendelea kufanya mambo makukwa katika jamii ambapo ni Benki kubwa inayoongoza kutenga fedha nyingi ili kuisaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya.
Wakati huo huo amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imejipanga kuhakikishaa inaanza ukarabati na Ujenzi wa vyoo yva Watu wenye mahitaji maalum katika maeneo mbalimbali Jijini humo sambamba na Serikali itaendekea kuhakikisha inajali mahitaji ya Watu wenye mahitaji maalum kwa kushirikiana na Jamii katika kuwasaidia.
Amesema Halmashauri hio iko tayari kushirikiana na Chama Cha Walimu Tanzania TWC Wilayani humo ili kutimiza lengo la kuwasaidia Watu wenye mahitaji hayo.
Kwa upande wake Meneja NMB Kanda ya Dr es salaam Dismas Prosper amesema Kila mwaka Benki hiyo inatenga asilimia moja Kwa ajili ya Watu hao ambapo wamekuwa wakifanya utaratibu Kwa muda wa miaka 7 hadi sasa.
Meneja Prosper amesema NMB inaingiza faida ya Zaidi ya milioni sita zinazotokana na Jamii hivyo wataendelea kuchangua huduma mbalimbali za kijamii kwani kiasi cha shilingi milioni Tatu wanazirudisha Kwa Watanzania ikiwa ni moja ya fadhila hivyo watahakikisha wanaendekea kuboresha huduma za Benki hiyo.
Amesema wanao wajibu wa kumuunga mkono Ras Dr Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu nchini ikiwemo Ujenzi wa madarasa na vitendea kazi hivyo wanao wajibu wa kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Amesema changamoto za sekta ya elimu NMB ndio kipao mbele chao hivyo wanatambua juhudi za Rais katika kusimamia na kufikisha elimu Mjini hadi vijijni. Hivyo ninamshukru Mkuu wa Wilaya katika kujitoa kushiriki nasi kwenye zoezi hilo sambamba na watumishi wa Umma katika utendaji kazi.
Baadhi ya Vifaa vilivyogaiwa Kwa Walimu na Wanafunzi wenye mahitaji maalum ni pamoja na chupa za Mafuta Kwa ajili ya kulinda ngozi zao, Kofia 60, Fimbo nyeupe 60, na Lenzi kwa ajili ya kusomea 60.


Hakuna maoni: