MILIKI GARI ZERO KILOMETERS KUTOKA NISSAN KWA GHARAMA NAFUU.


Dar es salaam.

Kampuni ya Nissan Tanzania imetoa rai kwa Watanzania kutokuhofia kununua Magari Mapya(Zero Kilometers) kutoka katika kampuni hiyo kwani wanaweza kununua na kulipa kidogo kidogo kupitia Bank mbalimbali walizoingia nazo mikataba.

Pia watajea wote watakaonunua magari kutoka Nissan Tanzania awataweza kupata huduma za ukarabati na matengezo mbalimbali kwa muda wa miaka mitatu.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Mauzo Mkuu wa Kampuni hiyo Edwick Mwamba wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye maonesho makubwa ya kibiashara yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

“Watanzania waache uoga ,sisi kama kampuni tunashirikiana pia na Mabenki ambayo yanaweza kutulipa sisi kama kampuni halafu mteja anachukua gari na kuendelea kuilipa Benki kidogokidogo mpaka atakapomaliza deni laki” amesema Edwick

Aidha amesema kuwa kuna dhana kuwa magari mapya (Zero Kilometers) yanagharama kubwa hali ambayo sio kweli kwa kampuni yao kwani wanazo bidhaa zenye gharama nafuu amambazo Mtanzania anaweza kuzimudu.

Pia Bi huyo wa Nissan Tanzania amesema kuwa Kwa sasa serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka Mazingira rafiki ya kibiashara hivyo Watanzania wakiamua na kuacha uoga wanaweza kumiliki magari mapya kutoka kampuni ya Nissan Tanzania.

Amebainisha kuwa kampuni hiyo inauza magari aina tofauti tofauti kama vile Pickup Navara,Station Wagon Y62(V8) Terra ,SUV Magnite.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.