SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi nchini, kuhakikisha huduma za bima tofauti zinawafikia wananchi wengi zaidi hususa ni wale waliopo maeneo ya vijijini.
Pia, wadau wa sekta hiyo wametakiwa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa zinazopatikana katika bima hizo.
Hayo yamebainishwa na waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Saada Mkuya, wakati wa uzinduzi wa taasisi ya FIRST UNITED TAQAFUL, inayojihusisha na utoaji wa huduma za bima zinazofuata misingi ya dini ya kiislamu, uliofanyika jijini dar es salaam, huku akizitaka taasisi za bima nchini, kujikita zaidi katika matumizi ya teknolojia za kisasa kuboresha huduma hizo.
"Serikali inatambua ukweli kwamba Sekta ya Bima ni sekta kubwa za kiuchumi ambazo zitasaidia nchi yetu kudumisha hali ya kipato Cha kati wananchi"
"Huu inaweza kupatikana kama tutapitia maendeleo na mikakati maalumu ya kuongeza watoa huduma ya Bima za kawaida, Bima za Taqaful pamoja na Bima za maisha"
Aidha alisema Moja ya malengo ya mikakati ya sekta ya nchini ni kuhakikisha tunakuwa na Bima mpya mpaka kufikia mwaka 2030.
"Kufikia malengo hayo yaliyowekwa ni muhimu kwa Mamlaka ya usimamizi wa Bima kuongeza hatua zaidi"
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya First United Takaful Abdulnassir Mohammed alisema lengo kuu la bima hiyo ni kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma za bima zinazofuata sharia ambapo huduma hizo zitafuata misingi ya ushirikiano na kuzingatia kanuni za uwazi, uadilifu, uwajibikaji pamoja na kukidhi mahitaji ya imani
Naye mkuu wa kitengo cha KCB Sahal Banking Amour Muro alisisitiza kuwa benki hiyo imekuwa ikisimamia ajenda ya ushirikishwaji wa kifedha kwa wananchi wote kwa kuhakikisha huduma zote za muhimu zinawafikia ikiwa ni pamoja na kuanzisha kitengo maalumu kinachotoa huduma za kibenki zinazofuata sheria za kiislamu
Pia aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuona mahitaji hayo na kutoa miongozo 2022 mwezi wa 5 ambayo kwa sasa imeanza kuonyesha matunda yake kwakuwa na kampuni hizo 2.


Hakuna maoni: