Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Gilbert Kalima (MNEC) ameshiriki katika Maadhimisho ya Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.
Katibu Mkuu Wazazi, Ndugu Kalima, alishiriki Maadhimisho hayo katika Wilaya ya Mpwapwa Jimbo la Mpwapwa, alifungua Kigoda cha Wazazi katika Kijiji cha Igojiwani Kilichopo Kata ya Mima.
Alishiriki upandaji wa miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika shule mpya ya Sekondari ya Mima yenye madarasa manne (4) na ofisi mbili (2) ambapo kwa kusapoti ujenzi huo aliahidi kuchangia Shilingi Milioni Moja (1).
Aidha Katibu Mkuu Wazazi, Ndugu Kalima, alishiriki katika mkutano wa hadhara na wanachama wa CCM, jumuiya zake na wananchi uliofanyika kwenye Kijiji cha Mima Kata ya Mima katika Jimbo la Mima, aliwapongeza wananchi hao kwa umoja na mshikamano walionao unaopelekea kufanya maendeleo kwa pamoja.
Aliwapongeza wanachama wa CCM na wananchi kwa jitihada waliyoonyesha katika ujenzi wa Sekondari mpya ambayo ikikamilika itawaondolea kadhia wanafunzi kutembea kilometa 9 kufuata shule nyingine ya sekondari ilipo ambayo ndio wanayotumia hivi sasa.
Aliwataka wananchi kuendelea kudumisha amani na kuimarisha ushirikiano kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo katika kata hiyo, amewausia uchaguzi wa serikali kuhakikisha CCM inashinda katika vijiji hivyo kwa maslahi mapana ya maendeleo yao, Kata, Jimbo na Nchi kwa ujumla.
Alipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza kwa vitendo maendeleo kwa wananchi ambayo inawajali watu wake kwa kuhakikisha wanapata huduma zote stahiki za kijamii.
Jumuiya ya Wazazi Taifa imeshiriki Maadhimisho ya Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa CCM Tangu Kuanzishwa kwake kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika Mkoa wa Dodoma kwa viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo.

Hakuna maoni: