COSTECH YAJIZATITI NA MABADILIKO TABIA NCHI,WAANZA KUTEKELEZA PROGRAMU HII.


Na Karoli Vicent,

Dar es salaam.

IMEELEZWA kuwa Athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi zipo mbioni kupata ufumbuzi baada ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kuanza kutekeleza programu ya utafiti wa mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhili wa nje.


Programu hiyo inatajwa kuwa suluhu ya changamoto ambazo ni zao la mabadiliko ya tabia ya nchi kama ukame ambao unaathari kwa jamii ikiwemo kuvunjia kwa ndoa kutokana na kufuata maji umbali mrefu, athari kwa mifugo, kilimo, ambapo kiujumla changamoto zinakumba karibu kila sekta.


Kutokana na hilo Costech inaendesha mchakato wa kuwapata watafiti nchini ambao watakuja na maandiko yenye mwarobaini wa changamoto hizo kupitia ufadhili wa Serikali ya Sweden (Sida) na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Norway (Norad).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya tume hiyo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu amesema wanahitajika watafiti nchini ambao watakuja na utafiti jumuishi ili kuleta suluhisho ya changamoto hizo.


Aidha,Dk Nungu, amefafanua kuwa kupita programu hiyo itachagiza sekta ya sayansi na teknolojia kwa kuleta teknolojia bunifu na elimu ya kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko hayo kwenye sekta mama ambazo zinategemewa katika uboreshaji wa huduma za jamii na ukuaji wa uchumi wa nchi.


"Mabadiliko ya tabia ya nchi ni mtambukwa hivyo watafiti tunategemea wawe na ubobezi wa sekta husika mfano kilimo, afya, ufugaji, mtu akisema atatatua changamoto hizo kupitia Tehama awe anafahamu kwa kina.


"Watafiti waeleze ni kwa jinsi gani teknolojia watakazokuja nazo zitawafikia wananchi na jinsi gani tafiti zao zitachangia katika kuboresha sekta zetu," amesema Dk Nungu.


"Miradi ya utafiti itakayofadhiliwa inategemewa kugharamiwa kati ya Sh220 hadi 600 milioni kwa kila tafiti ambapo ndani ya miaka minne matokeo ya suluhisho hizo utakuwa yanatekelezwa.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.