PROF LWAITAMA;WAZEE NDIO CHIMBUKO LA FIKRA,MAARIFA,HEKIMA NA BUSARA.

 



Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Ngome ya wazee ACT-Wazalendo wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuiunganisha jamii na kuwa moja licha ya kuwepo kwa mitazamo tofauti jambo ambalo litaepusha mifarakano ndani ya chama,vyama vya siasa na jamii kwa ujumla


Wito huo umetolewa leo Machi 1/2024 na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA Prof Azaveli Lwaitama Wakati akifungua Mkutano wa pili wa Ngome ya Wazee ACT-Wazalendo,ambapo amesema wazee kazi yao kubwa ni kutafakari jambo kabla ya kutenda na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi.

Ameongeza kuwa nadharia nyingi hutokana na mapokeo, wazee wameona mengi na wanajua vingi vinavyowafanya kuona mbali hivyo huweza kuonya mambo mabaya kabla ya kutokea.

"Kazi ya wazee katika chama na jamii ni kupunguza moto wa vijana".

Aidha amesisitiza kuwa hakuna chama kimoja kitakacholeta ukombozi kunapaswa kuheshimiana kwa vyama vya upinzani ili kuweza kuweza kushika dola.

Kwa upande wake Askofu mwamakula amesema viongozi wadini wamekuwa wakionya mambo mbalimbali yanayooneka kutoenda vizuri hususani yeye amekuwa akionya mara kwa mara kwa pande zote iwe vyama vya siasa na serikali.

Amewataka wagombea watakao shinda kwenye uchaguzi huo kuwatumia washindani wake na wazee wengine kuwashauri katika utendaji wao na watambue kuwa wao sio wenye hekima zaidi bali wamepita ili kuwatumikia wengine.

Sheikh issah ponda amesema jambo la kutumika na umma ni swala kubwa mno wazee ni watu wakuheshimika sana katika jamii kwakuwa wanauzoefu mkubwa katika maswala mbalimbali.

"Kikao cha leo kinawezekana kikaomekana kidogo lakini nikikao kikubwa zaidi naweza kusema kuwa kikao hiki ndio kikao kikuu cha chama.Wazee ndio nguzo kuu ya kufikiri ni kisima cha fikra na busara".

Aidha mkutano huo pamoja na mambo mengine unalenga kufauchaguzi wa viongozi wa Ngome hiyo.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.