DODOMA.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ni Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mkutano wa Sita wa Mafundi Sanifu Tanzania kwa mwaka 2024 “6th Engineering Technicians Day” jijini Dodoma, leo tarehe23 Mei 2024.
Mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu “Matumizi ya Akili Mnemba kuongeza ufanisi: Kuimarisha Mafundi Sanifu kwa changamoto zinazoibuka” na umehudhuriwa na mafundi Sanifu wapatao 800 na wengine 50 wakifuatilia mkutano huo kwenye mitandao.
Viongozi wengine walioshikriki katika Mkutano huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Kaimu Katibu Mkuu wa Ujenzi, Richard Mkumbo, Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya ERB pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Hakuna maoni: