AKIBA BANK YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUZINDUA VIUNGA VILIVYOBORESHWA VYA INDEPENDENCE SQUARE, DODOMA.

DODOMA.

Akiba commercial Bank Plc tawi la Dodoma laadhimisha siku ya mazingira Duniani (World Environmental Day) kwa kukabidhi rasmi awamu ya pili ya uboresha wa viwanja vya independence square.

Katika Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shakimweri, wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari, na wafanyakazi wa Benki ya Akiba Commercial.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa tawi la Dodoma la Benki ya Akiba, Bi. Upendo Makula, alisisitiza jitihada za Benki hiyo katika kujitolea kuhifadhi na kutunza mazingira, sambamba na kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu, isemayo “Our Land, Our Future” - “Ardhi Yetu, Mustakabali Wetu,” ambayo imebebwa na mada kuu ya “Land restoration, desertification and drought resilience” ambayo inalenga urejeshaji (utunzaji) wa ardhi, kupambana na uzalishaji wa majangwa, na ukame. 

Aidha Alikumbusha na kusisitiza juu ya wajibu wa pamoja wa kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuhakikisha dunia inabaki kuwa mahali salama pa kuishi kwa sasa na vizazi vijavyo.

Bi. Makula alieleza kuwa Benki ya Akiba inashiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kwa namna mbali mbali kuanzia kupitia huduma zake na ushiriki wa katika shughuli mbali mbali za kijamii. Aliainisha kuwa Benki hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi kwa kuboresha huduma zake za kidijitali, zikiwemo Akiba Mobile, Akiba Wakala, kadi za VISA, taarifa za kielektroniki (E-statement), na huduma za benki Mtandao (Internet Banking).

"Huduma hizi si tu kwamba zinapunguza matumizi ya karatasi, bali pia huleta urahisi na uhakika, hivyo kukidhi mahitaji ya soko kwa ufanisi. Aidha, benki hiyo inatoa huduma mbalimbali kama mikopo, akaunti, na bima, zinazowafikia wateja tofauti kuanzia mtu binafsi hadi makampuni makubwa na taasisi za serikali".

Vilevile, Bi. Makula alibainisha kuwa Akiba Commercial Bank inashiriki kikamilifu katika shughuli za jamii za kuhifadhi mazingira kama sehemu ya Sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Mfano halisi ni jitihada zake za muda mrefu za kutunza na kuboresha viwanja vya Independence Square huko Dodoma, jukumu ambalo limekuwa likitekelezwa kwa zaidi ya miaka kumi.

"Juhudi hizi zinaonyesha nia thabiti ya benki hiyo ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya urithi bora wa vizazi vijavyo.Tukio hilo pia lilihusisha kukata utepe na kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vilivyoboreshwa na Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Wilaya Alhaji Jabir Shakimweri ya Dodoma". 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya aliipongeza Benki ya Akiba kwa juhudi na jitihada zake katika kuboresha na kuhifadhi mazingira. Pia ametoa rai kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa Akiba. Bi. Makula, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Silvest Arumasi, pamoja na uongozi na wafanyakazi wote wa tawi la Dodoma, alisisitiza nia ya benki hiyo ya kuendelea kusaidia uboreshaji wa mazingira na miradi mingine ya kijamii, hasa katika sekta za afya na elimu.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.