TCCS KUFANYA MAONESHO YA MIFUGO KUANZIA JUNI 14-26 MKOANI PWANI.

DAR ES SALAAM.

Chama cha Wafugaji Ng’ombe Kibiasgara (TCCS) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Bank ya Maendeleo ya kilimo ADB wanatarajia kufanya maonesho ya mifugo kuanzia Juni 14 hadi 16 mwaka huu 2024 katika viwanja vya Ubena Estate Chalinze Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 5, 2024 jijini Dar es Saalaam Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji ng'ombe kibiashara Naweed Mulla amesema lengo la maonesho hayo ni kusaidia wakulima na wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa wenye tija utakaosaidia jamii kujikwamua kiuchumi pamoja na kuongeza pato la Taifa.

Ameongeza kuwa zaidi ya wadau wa 300 wa ufugaji wanatarajiwa kushiriki Maonesho hayo ambayo yatawawezesha wafugaji, wasindikaji na wadau mbalimbali nchini kushawishi sera za maendeleo na kukuza uzalishaji wa mifugo endelevu kwa njia ya kuwajengea uwezo na mitandao.

"Maonesho haya yana nia ya kuwezesha Jukwaa Madhubuti la Kitaifa la wafugaji, wasindikaji na wadau katika mnyororo wa thamani ya ili kuendeleza sekta hiyo kwa mbinu bora endelevu za kiuchumi na kimazingira"

Kwa upande wake Kaimu Mkurugezi Idara ya Mipango, Ushauri na Mahusiano ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Mkani Waziri amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja kushirikiana na TCCS ili kuona namna wanavyoweza kuleta mageuzi katika tasnia ya ufugaji.

Ameelezaa kuwa wamekuwa washiriki wakuu katika tasnia ya ufugaji ili kuhakikisha watanzania wanafuga kwa tija na kuweza kupata kipato na kukuza uchumi wao.

Waziri amefafanua kuwa mpaka sasa wametoa mikopo kwa wafugaji shilling bilioni 38 ambayo imewanufaisha wafugaji 8,688 katika mikoa 21.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoani Pwani, Ngobere Msamau amesema kuwa kupitia maonesho hayo wanatarajia kupata elimu ambayo inakwenda kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa na kuondokana na ule wa kienyeji.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.