BODI YA MIKOPO YAZINDUA KAMPENI YA FICHUA.

Na Mwandishi wetu,

Dar es salaam.

Bodi ya Mikopo Tanzania HELSB imewaomba wananchi kuwafichua wanufaika wa mikopo waliohitimu vyuo muda mrefu na wana vipato na ajira ambao mpaka sasa wamekaidi kurejesha fedha walizokopeshwa ili kusaidia wengine nao waunufaike.

Ombi hilo limetolewa leo Juni 28,2024 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini(HELSB),Dkt Bill Kiwia,wakati wa uzinduzi wa kampeni fichua "kuwa hero wa madogo" ya kizalendo itakayoendeshwa kwa miezi miwili nya ambapo kila mtu ambaye anamfahamu mnufaika wa mikopo hiyo na ana kipato au ameajiriwa na taasisi, kampuni ataombwa kutoa tarifa ya huyo mhusika kwa kutuma majina yake yote matatu na Chuo kikuu alichosoma na mahali alipo ili afuatiliwe.

" Tunafahamu kuwa wateja wetu wadaiwa sugu ni wengi wengine wameajiriwa na taasisi binafsi, makampuni huku wengine wakiwa wamejiajiri na wanavipato hawakumbuki fadhila walizotendewa wakiwa kwa kupewa mikopo wakiwa vyuoni lakini hawataki kurejesha kidogo kidogo fedha mikopo yao hivyo kampeni hiyo wananchi wote wasaidiae kuwafichua ili warejeshe na wengine nao wanufaike"amesema Dk Kiwia

Sanjari na hayo amebainisha kuwa hali ya urejeshwaji mikopo ni nzuri ambapo mpaka sasa wanakusanya bilioni 15 kwa mwezi sawa na 70% ikilinganishwa miaka iliyopita hivyo kupitia kampeni hiyo ya itasaidia kupatikana kwa fedha ambazo zilikopwa na kupunguza malalamiko ya baadhi ya wanavyuo kusema boom wanalopewa haliwatoshi kulingana hali ya maisha .

Sanjari na hayo kiasi wanachokidai ni kikubwa trilion 2.1 na hadi sasa wamekusanya trilion 1.3 bado bilioni 600 hivyo fedha ni bilioni 200 kwa wanafunzi elfu 50  

Aidha wito umetolewa kwa wananchi wote ikiwemo mama,kaka,dada na wanafunzi ambao walishawahi kunufaika na mikopo hiyo kuwa wazalendo kuwafichua wale ambao hawajarejesha kwa kutuma ujumbe kwa simu no,0739665533, kupiga simu 0736665533 wakituma majina yao matatu vyuo walivyosoma na mahali walipo kwa sasa hii isaidie wengine nao wanufaike kwani kuna wanafunzi wasio na wazazi wote wawili , wengi familia zao ni za vipato vya chini na wameshindwa kusoma kwa kukosa ada .

Kwa upande wake,Mkurugenzi urejeshaji na urejeshwaji mikopo CPA George mziray ,amesema wanafunzi wote waliohitimu kidato cha sita na wanahitaji kwenda vyuoni dirisha la mikopo limefunguliwa waombe kupitia mtandao.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.