JUKWAA LA WAPIGAPICHA NA VIDEO WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI.




Na Mwandishi wetu


JUKWAA la Wapiga picha na wachukua video za matukio wametakiwa kuzingatia weledi ,uzalendo, na mila na desturi za taifa ili kuepukana na sintofanfamu katika jamii kupitia shughuli zao 

Agizo hilo amelitoa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salim Mtambule leo Juni 25, 2024 Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la pili la wapigapicha na wachukua video ambapo amewasisitiza kuwa kabla ya mtu kufanya shughuli hiyo aangalie je video au picha ina maadili mema katika jamii ikionekana tafsiri yake itakuwaje inajenga au inabomoa maadili hivyo weledi na ubora ni vitu muhimu .

"Licha ya changamoto mnazopitia katika utekelezaji wa majukumu yenu msikate tamaa endeleeni kuwa wabunifu zaidi kwani serikali inatambua kazi kubwa mnayoifanya ninyi ni watu wa pekee kwani suala la picha au video linaweka kumbukumbu ya muda mtefu akitolea mfano matukio mengi ya historia ya Taifa hili yalihifadhiwa kupitia picha kizazi hadi kizazi kinaendelea kujifunza " amesema Mkuu wa Wilaya

Sanjari na hayo Mkuu wa Wilaya amesema kuna umuhimu wa serikali kulitambua jukwaa hilo kwa kuanzisha Mashindano ya wapiga picha na wachukua video huku kukiwa na tunzo mbalimbali kama ilivyo katika tasnia nyingine ili kuleta hamasa na kutambua mchango wa wadau hao katika jamii.

Awali Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Rajabu Mtacha ameomba taasisi mbalimbali kuwapatia elimu ikiwemo semina za bima,Uwekezaji,Afya, wadau hao kwani wamesahaulika japo ni kundi muhimu na limekuwa likifanya kazi kubwa na gumu za serikali na binafsi .

"Lengo la kuundwa Jukwaa hili ni kutokana na kuona tumesahauliwa ukilinganisha na kazi zetu na vifaa tunavyovitumia kufanya shughulia akitolea mfano utakuta mtu anabeba vifaa vyenye thamani ya Milioni 40 havina hata bima hata itakapotokea dhara lolote ajali hakuna fidia yeyote hivyo watu wa Bima wakitupa elimu ya kukatia vifaa vyetu bima itasaidia sana sisi tutakuwa wateja wao vilevile NSSF kuhusu kuwekeza na UTTAM " amesema Mwenyekiti wa jukwaa

Kwa Upande wake Mpiga picha Nguli kutoka kampuni ya Desktop production Limitedi(DTP ) Hanif Abdulrasul amebainisha kuwa yeye alinunua kamera yake mwaka 1984 na kuanza kujifunza ujuzi huo kutokana na kufanya kazi kwake kwa ubora na weledi alibahatika kupata tenda ya kumpiga Aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje Marehemu Bernad Membe, Makamu wa Rais Philop Mpango ,Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na picha ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani inayouzwa na Habari Maelezo yeye ndiye aliyeipiga .

Hivyo amewashauri vijana wanaochipukia kuipenda hivyo kazi wawe wastahimilivu wanapopata tenda ya kazi wajitahidi kujenga mawasiliano ya karibu na mteja siyo wakimaliza kazi wanafuta namba kabisa na hali hiyo inapelekea kujikosesha kazi wenyewe kwani shughuli ni nyingi kuna sikukuu za kuzaliwa sherehe za kanisani hivyo weledi na ubora kazi nzuri zenye ufanisi itasaidia kuondokana na ukata


Aidha wadau wa jukwaa hilo walio shughuli zao kubwa ni kuchukua video au picha kwenye matukio ikiwemo harusi ,ibada makanisani au misikitini, misibani,uzinduzi , ziara za viongozi , kutengeneza documentari ,kutengeneza movie,





Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.