Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam.
TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wametoa viti mwendo 250 kwa watoto wenye ulemavu ili kuwasaidia kutembea hususani kwenda shule.
"Kuna Wanaume ni Wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikia kuwa kana kuwa mtoto mwenye Ulemavu si wake, lakini mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai mwanamke kuwa mtoto ni wake"Alisema Mwenyekiti wa Taasisi Ongea na Mwanao Steve Nyerere.
Nyerere Aliongeza kuwa Hali ya Mtoto Mwenye Uhitaji haimzuii mtoto huyo kupata Elimu.
"Sisi tunahitaji kupeleka Mahitaji kwa Wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono"Asisitiza Steve Nyerere.
Kwa upande wake Katibu wa taasisi hiyo Evonsherry Monalisa amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na kubakisha mikoa miwili kwa jili ya Viti mwendo kwa wahitaji.
Amesema kampeni ya "Baskeli ya Shule ya Mama" inalenga kumsaidia mtoto mwenye uhitaji kupata Elimu.
"RaisDk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni" Alisema Evon Sherry.
Hakuna maoni: