Na Mwandishi wetu,
Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida ameziomba mamlaka za Serikali kuudhibiti mtandao wa X maarufu kama Twitter kwa kuufungia baada ya mmiliki na waendeshaji wa mtandao huo kuruhusu maudhui ya mapenzi ya jinsia moja.
"Kwanza hata jina lenyewe tu linalotumika limekua na maudhui yanayoendana na masuala ya ponograph, walibadilisha jina na kuutia X ili kutuandaa kisaikolojia kwani hata picha chafu zinafahamika kwa jina hilo ili watakaporuhusu watu wasishtuke lakini hapana si sawa kuendelea na huo mtandao nchini kwetu ukizingatia maadili yetu,watoto wengi wanatumia simu na wanaingia kwenye mitandao, hivyo sio vizuri kutimika nchini kwetu"amesema Kawaida.
Pia amesema wao hawana shida na mtandao huo ikiwa wataondoa maudhui yake basi uendelee kutumika ila kama haiwezekeni basi vyema serikali ikaufungia kutokana na kupandikiza tabia zisizofaa miongoni mwa wanajamii ya Kitanzania.
Aidha amewataka vijana wote nchini pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kukemea vikali juu ya matumizi ya mtandao wa X (Twitter) nchini kutokana na kubadilika kwa maudhui ya mtandao huo ikiwa ni pamoja na kuacha kabisa kuutumia.
Hakuna maoni: