DAR ES SALAAM.
Jumuiya ya Wachumi Tanzania (EST) imewatakawanachama,wachumi,pamoja na wadau wa uchumi nchi kushiriki katika Mkutano mkuu utakaoambatana na kongamano la la mwaka la uchumi utakaofanyika siku ya Tarehe 12/07/2024 katika Ukumbi wa Bank kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es salaam.
Kongamano hilo la mwaka linaloongoza kwa wachumi nchini, linalenga kuwavutia wachumi wa wakuu wa kielimu,kisera, na soko kujadili maswala yanayohusu uchumi wa Tanzania.Pia kongamano hilo litatoa wasaa kwa wachumi nchini na kutoka diaspora ili kuja na masuluhisho madhubuti ya matangamano na changamoto za Maendeleo zinazoikabili Tanzania.
Pia wataendesha program za kuimarisha uwezo wa wachumi hiyo ikiwa ni mahususi kwa wachumi wachanga kuimarisha ujuzi wao ili uweze kumsaidia katika kufanyakazi mbalimbali ikiwemo kutengeneza maandiko,kuibua miradi yenye matokeo chanya kwa jamii,kuandaa taarifa za kiuchumi,kufanya tafiti,kuratibu mipango ya kiuchumi,kuandaa majukwaa ya majadiliano.
"Taasisi yetu inajukumu kubwa la Kukuza mijadala ya kiuchumi nchini,mitazamo ya kiuchumi/ushauri wa kiuchumi unatofautiana na mwingine kwahiyo ni lazima kuwe na mijadala ya mara kwa mara ili kuwa na mawazo/makubaliano ya pamoja juu ya uchumi wetu" Amesema Mwambe na kuongeza kuwa
Aidha ametaja Malengo Makuu ya mkutano huwa kuwa ni kupata majawabu katika changamoto zilizopo katika jamii,"haitakuwa na maana wachumi tupo alafu tunafanya mambo bila kuzingatia ushauri wakitaalamu".
Kadhalika kupitia mkutano mkuu huo wanachama watapata wasaa wa kufanya uchaguzi wa safu ya uongozi mpya itayoongoza taasisi kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba ya EST.
Pia mwambe amesema katika mkutano na kongamano hilo wanatarajia kuhudhuliwa na Watu 300-500 ambapo wamealika wazungumzaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Sambamba na hayo wamenawaalika vyama vyote vya kitaaluma ikiwa ni pamoja na Bodi ya manununizi,wahasibu,bodi za wakandarasi,bodi ya mainjinia,bodi ya biashara,chama cha wanasheria,sekta za umma karibu 267, sekta binafsi,cti,tccaa,umoja wa bank Tanzania na Taasisi zingine pia wanakaribisha mtu mmoja mmoja.
Pia Wamewataka wachumi wote kushiriki katika kongamano hilo kwa kujisajili kupitia www.wachumi.com ambapo watakutana na link ya kujisajili kushiriki kongamano hilo.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Majukumu ya Jumuiya ya wachumi Tanzania katika maendeleo ya uchumi wa Taifa
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.
Hakuna maoni: