RAIS SAMIA AOMBWA KUSAIDIA BIMA YA AFYA KAYA MASIKINI.

Na Selemani Msuya

MBUNGE wa Viti Maalum (CHADEMA), Sophia Mwakagenda amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuunga mkono kampeni yake ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuwapatia bima ya afya zaidi ya watu 2,000 kutoka familia masikini nchini.

Mwakagenda ametoa ombi hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mapambano ya hisani yanayotarajiwa kufanyika mkoani Geita Julai 28 mwaka huu.

Mapambano hayo yatashirikisha mabondia marufu Karim Mandonga, Mada Maugo, Ibrahim Class na wengine ambapo fedha zitakazopatikana zitatumika kulipia bima ya afya kwa watu 2,000 wanaotoka familia masikini.

Mbunge huyo amesema kampeni hiyo inaenda kugusa jamii ya Kitanzania, hivyo anamuomba Rais Samia kumuunga mkono kwa kulipia bima za Watanzania 300 wanaishi katika umaskini.

“Pamoja na Rais Samia, pia namuomba Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko, Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Ju

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.