JWTZ KUFANYA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 TOKEA KUANZISHWA KWAKE 1964.

 


Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajiwa kufanya maadhimisho ya miaka 60  tokea kuanzishwa kwake mwaka 1964 ambapo September Mosi, 2024 mwaka huu litatimiza umri huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Habari Jijini Dar es salaam mapema hii leo Julai 03/2024 wakati akitoa taarifa ya maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ) ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo Luteni Kanali Gaudentius Ilonda ambapo amesema Jeshi limeamua kufanya maadhimisho ya kipekee na ya aina yake ambapo yataanza Julai 25/2024 na yatafikiwa kilele chake siku ya tarehe 01/09/2024.

Luten Kanal Ilonda amesema katika kusherekea maadhimisho hayo ya miaka 60 ya JWTZ kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo Mazoea ya kivita,kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutoa matibabu bure kwa wananchi na ukizingatia kuwa jeshi hilo lipo kwaajili ya wananchi.

Ameongeza kuwa Kuanzia Julai 25/2025 hadi Agosti 23/2024 Jeshi litafanya zoezi la kivita liatakoloshirikisha kamandi zote za jeshi ikiwemo jeshi la anga, ardhini, majini,jeshi la akiba na vikosi maalumu.

Zoezi hilo litafanyika katika maeneo mbalimbali Nchini ambapo ameyaja maeneo hayo kuwa ni Dar es salaam,Pwani,Tanga na Morogoro hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kutokuwa na taharuki wakati wa mazoezi hayo ya kijeshi yatakapofanyika

"Katika mikoa hiyo tutashuhudia mapigo mbalimbali ya ardhini,angani na baharini yakiwa yanafanyika na wananchi watapa fursa ya kushuhudia kwa walioko karibu na kwa wa mbali wataona kupitia vyombo vya habari".

Sambamba na zoezi hilo , Jeshi litakuwa na mambo mbalimbali katika kusherekea maadhimisho hayo ambapo kutawakuwa na mashindano ya utamaduni ya Mkuu wa Majeshi.

"Kimsingi mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza, na kwa maono yake Mkuu wa Majeshi CDF Jacob Mkunda amelenga yafanyika ili kuenzi na kudumisha utamaduni wetu".

Pia kutakuwa na mashindano ya Mkuu wa majeshi CDF Cup ambapo yatakuwa yanajumuisha michezo mbalimbali.

Pia kutakuwa na zoezi la kutoa Huduma mbalimbali kwa wananchi ambapo kutakuwa na utoaji wa matibabu bure ambapo yatafanyika katika hospital zote za kanda za jeshi ambazo ni Hospital ya kanda ya Arusha, mwanza, Mbeya Tabora na Zanzibar.

"Hii ni kusherekea kwa pamoja na wananchi kama mnavyojua wanahabari jeshi hili ni la wananchi tunapotimiza miaka sitini tukiwa na umoja na amani hatuna budi kuwashuru".Amesema Luteni kanali Ilonda.

Katika utoaji wa huduma bure za matibabu Watatoa huduma zifwatazo;-kupima na kutoa ushauri juu ya magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza ikiwemo kisukari,UKIMWI, shinikizo la damu,saratani ya matiti,tezi dume,huduma za maabara na damu salama lengo likiwa ni kuchangia damu,duhuma ya magonjwa ya dharula na matibabu mengine.

Pamoja na hayo yote yaliyopangwa kufanyika na jeshi yatahitimishwa na Gwaride rasmi litakalobeba sura ya miaka sitini pia litaambatana na onyesho maalumu kuonesha jeshi lilipotoka tokea mwaka 1964.

Aidha pia katika kuadhimisha maadhimisho hayo Serikali kupitia JWTZ na Serikali ya China kupitia jeshi la ukombozi la watu wa China watafanya zoezi kubwa la kihistoria la kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja katika maeneo ya Dar es salaam na Pwani ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 29/07/2024 na kuhitimishwa tarehe 11/08/2024.

"Zoezi litafanyika baharini kwa kutumia zana za kivita za baharini pia litafanyika ardhini ambapo zoezi hilo litashirikisha zana na vifaa mbalimbali ikiwemo ndege,magari,meli, zoezi hilo litafayika wazi wanachi wote wataona"Amesema Luteni kanali Ilonda.

Luten kanal Ilonda ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo pia watatoa matibabu bure kwa wananchi ambapo zoezi hilo litafanyiaka nchi kavu na baharini kupitia meli kubwa ikiwa ni sehemu pia ya utalii. meli kubwa ya matibabu itatia nanga Bandari ya Dar es salaam Julai 16/2024.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.