DAR ES SALAAM.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatajia kuzindua safari za Treni ya Mwendokasi SGR Dar es salaam hadi Dodoma Agosti 01 mwaka huu 2024.
Hayo yamebainishwa leo Julai 30, 2024 na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuekekea hafla ya uzinduzi huo utakaofanyika Agosti 1, 2024 jijini Dodoma.
Profesa Mbarawa ameeleza kuwa Serikali imelenga kupata faida katika huduma ya usafiri wa treni za Mwendokasi kupitia usafirishaji wa mizigo na sio kupitia abiria wa kawaida.
Amebainisha kuwa treni za SGR zinauwezo wa kubeba tani elfu 10 za mizigo sawa na maroli 500 kwa wakati mmoja hali itakayopelekea kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam,kuimarisha fedha yetu na kuongeza soko la ndani.
"Lengo la Serikali kujenga Reli ambayo ukiangalia ndani ya Nchi za Afrika sisi Tanzania ndio nchi pekee yenye mtandao mkubwa wa reli ya kisasa yenye Km 720 na kupitia reli hii Mizigo ndiyo itakayoleta faida kubwa na sio wasafiri wa kawaida," amesema Prof. Mbarawa na kuongeza,
"Mpaka sasa Serikali imetumia Dola Milioni 3.138 kukamilisha ujenzi wa reli huku shilingi Trillion 1.3 zimetumika kununua vitendea kazi vikiwemo mabehewa 89, seti 10 za vichwa vya treni ya mchongoko na vichwa 19 vya treni ya umeme,"
Hakuna maoni: