Na Mariam Muhando,
Dar es salaam.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli amemuomba Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha mapinduzi CCM komredi Amos Makala amfikishie Salam Rais Dr Samia Suluhu Hassani za kukamilisha miradi mbalimbali iliopo Jimboni humo.
Mbunge Bonnah ameyabainisha hayo katika Mkutano Uliowakutanisha Wananchi Jimboni humo katika Viwanja vya Liwiti Wilayani Ilala Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili Segerea.
Bonnah amesema Wilaya ya Ilala ni moja kati ya Wilaya inayoongoza katika ukusanyaji wa Mapato hapa Nchini hivyo amemuomba Katibu huyo awafikishie salama zao Kwa Rais ili aweze kuwatatulia Changamoto zao
"Tunakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo Maji, Umeme, barabara, na suala la mikopo kwa Wanawake iweze kurudishwa ili iweze kuwasaidia katika kujikwamia Kiuchumi", amesema Bonna
Hata hivyo amempongeza Rais Samia Kwa kuboresha miundo mbinu ya elimu na Afya ambapo waliletewa Zaidi ya Bilioni 6.8 zilizotumika katika Ujenzi wa Vituo mbalimbali vya Afya Jimboni humo.
Hakuna maoni: