VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUJIEPUSHA NA MIGOGORO.


Na Mwandishi wetu,

Dar es salaam.

Viongozi wa Vyama vya Siasa Nchini wetakiwa kushiriki katika mafunzo mbalimbali ya kisiasa ili kujenga uwezo wa kukabiliana na migogoro ndani ya vyama na hata kuepusha mipasuko.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijinili Dar es Salaam Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi mara baada ya kufungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini, yenye lengo la kujenga mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo.

Mafunzo hayo yamelenga katika maeneo mbalimbali imkiwemo kujifunza kuandaa Taarifaya fedha ya kuawasilisha kwa CAG,pamoja na kuandaa Matamko ya Mali za Chama hadi kufikia Mwezi Septema Mwaka huu.

 Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa ni Taasisi ya Umma hivyo vinapaswa kusajiliwa na kutenda Majukumu yanayotambulika kidemokrasia na kuachana na vurugu ambazo zinasababisha vyama hivyo kuwa na mpasuko.

 "Haya Mafunzo yatasaidia kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo Mogogoro ya ubadhilifu wa fedha za chama nakusababisha kuingia kwenye matumizi mabaya ya fedha za chama hali ambayo imekua ikiripotiwa mara kwa mara kwenye taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)amesema Jaji Mutungi.

Pia amevitaka vyama vya siasa kuwa vinara wa kujenga nchi na kwamba Tanzania sio nchi ambayo inapata utawala kwa mabavu bali ni demokrasia iliotukuka.

 “Mkifanya mema wafuasi wengi watawafuata,mkifanya maovu hakubna atakaewafuata,naomba sana nitoe wito kwenu muawambie wafuasi wenu waepukanae na migogoro na badala yake walinde amani ya Taifa”amesisitiza Jaji Mutungi

Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokratic Part (DP) Philipo Fumbo ameishukuru ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kwa kuandaa mafunzo hayo ,huku akibainisha kuwa vyama vingi vya upinzani havina ruzuku kutoka serikalini hali ambayo inachangia kushindwa kuajiri wahasibu na maafisa ununuzi nakupeleeklea migogoro ndani ya vyama kutokana na matumizi mabaya ya fedha.
Nae, Katibu Mkuu wa Chama Cha ACT - Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa migogoro ya vyama vya siasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya maridhiano na sio kutumia nguvu zisizofaa.

 "Ni kweli Migogoro inapasua vyama ,hivyo ni vyema vyama kutatua migogoro kwa njia ya maridhiano, tunaishukuru ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutuletea mafunzo haya ili kuondokana na Migogoro kwenye vyama vyetu vya siasa "Amesema Ado

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.