PROF. MKENDA AWATAKA WACHUMI KUFANYA TAFITI ZITAKAZO SAIDIA KUONGEZA AJILA KWA VIJANA.

 


DAR ES SALAAM.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka wachumi kuendelea kufanyatafiti zitakazochangia kuongezeka Kwa ajira Kwa vijana ambazo zitachangia kukua Kwa uchumi.

Prof. Mkenda ametoa wito huo Julai 12, 2024 Jijini Dar Salaam wakati akifunguaKongamano la Pili la Mwaka la Uchumi la Jumuiya ya Wachumi Tanzania 2024. (EST) akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango.

Prof Adolf Mkenda Amesema mageuzi ya uchumi yanahitaji kuwekeza katika nguvu kazi ya Taifa hasa kundi la Vijana linalotegemewa kushiriki katika sekta mbalimbali za uzalishaji pia amesema wachumi wananafasi kubwa ya kuhakikisha wanachambua masuala mbalimbali ya kiuchumi nchini na Kutoa ushauri Kwa uchambuzi wa kitaalam Kwa kadri inavyowezekana pamoja na kuongeza ubora wa uelewa wa uchumi.

"wakati tunafanya tafiti zetu tufanye katika Mazingira yetu na tuelewe changamoto ambazo sisi zinatukabili kama Taifa na hapo itasaidia katika kuratibu mbinu za kukabiliana na chanangamoto hizo"amesema Prf Mkenda na kuongeza,

"nilikuwa kwenye mkutano mwingine hapa juzi na nilisikia mada inayozungumzia kuwa na wazee wengi katika nchi,na ni suala ambalo tunaelekea huko lakini kwetu kubwa zaidi ni kuwa na vijana wengi ambao watakuwa na matarajio makubwa ya kupata ajira au kujiajiri na endapo tutajenga uchumi utakaozalisha ajira kwa hao vijana tutajenga uwezo Mkubwa wa kuhakikisha tunawapa mafao pindi watakapozeeka na hapa ndipo wachumi wanaweza kushauri vyema"ameongeza.

Aidha amesema Serikali inatekeleza juhudi mbalimbali katika kusaidia maendeleo nchini pamoja na kufanya mageuzi makubwa ya elimu na uboreshaji wa miundombinu ili kuwezesha utolewaji wa elimu bora kwa Watanzania ambayo itachangia kuongezeka kwa wabobezi wa uchumi watakaoliinua Taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la wachumi Tanzania Dkt Tausi Kida akizungumza Kuhusu kongamano hilo la pili la mwaka la Jumuiya ya wachumi Tanzania amesema kongamano hilo pia linaambatana na mkutano mkuu wa mwaka wa jumuiya ambao utatoa fursa ya kuchaguliwa Kwa safu Mpya ya uongozi.

"Leo tumekusanyika hapa tuna mada mbalimbali zitajadiliwa Kwa mustakabali wa uchumi na Kubwa leo tutachagua viongozi wetu akiwemo Mwenyekiti na Makamo mwenyekiti pamoja na wajumbe ambao wataingia kwenye Baraza kuu"amesema Dkt Tausi.





Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.