FCS NA TCRA CCC WAINGIA MKATABA KUSHIRIKIANA KUIMARISHA HAKI ZA WATUMIA HUDUMA ZA MAWASILIANO NCHINI.





Na Emmanuel Kawau,

Dar es salaam.

Foundation for Civil Society (FSC) Na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) hii leo Agosti 06/2024 zimetiliana saini makubaliano ya miaka mitatu yenye lengo la kuimarisha juhudi za kulinda haki za watumiaji wa huduma katika sekta ya mawasiliano Nchini.

Akizingumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema Ushirikiano huo ni kielelezo cha nia thabiti ya kuwezesha watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kukuza haki zao katika ambapo Ushirikiano huo pia unalenga kujenga mazingira bora katika soko kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ili wawe wenye taarifa sahihi na kulinda stahiki.

Ameongeza kuwa ubia huo unalenga kuhakikisha haki na wajibu katika kutoa huduma kwa watumiaji na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi wanaponunua na kutumia bidhaa na hudua za mawasiliano,kulinda haki za watumiaji.

"Kwa miaka mingini FCS imekuwa ikisisitiza maendeleo yaliyojikita katika kuwanufaisha wananchi na kuwaweka mbele, nafasi yetu na utayari weru katika ulinzi wa watumiaji wa huduma na bidhaa vinatokana na dhana hii na tuna lengo la kukuza mifumo thabiti ya kulinda watumia wa huduma na bidhaa kwa kuzishirikisha asasi za kirai" Amesema Rutenge.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) Merry msuya amesema Lengo la mashirikiano hayo ni kuboresha uwezo wa watumiaji wa huduma za mawasiliano ambapo kila mtu ni mtumiaji wa huduma hizo.

"Ukuaji wa teknolojia umefanya watumiaji kuwa na huduma nyingi katika sekta ya mawasiliano ambapo katika karibia kila sekta wanatumia mawasiliano ikiwemo sekta ya afya,elimu,uzalishaji, na nyinginezo wote wanatumia mifumo ya mawasiliano katika utoaji huduma zake".

Ameongeza kuwa Kupitia huduma za mawasiliano wanataka wananchi waweze kutumia huduma hizo kujipatia kipato na kuweza kuvumbua mbinu mbalimbali za kuwaweza kupata fursa za kiuchumi kupitia mawasiliano.


"Tunataka kila mtumiaji aweze kujua haki zake, akikwama ajue aende wapi na wapi ili aweze kupata utatuzi wa swala lake,".

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.