AKIYEKUWA MHASIBU MSAIDIZI WA NSSSF SACCOS ASHTAKIWA KWA RUSHWA.

 


DAR ES SALAAM.

Shauri la Uhujumu Uchumi namba 26102/2024 Jamhuri dhidi ya *Robert Stuart Konni*- Aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa NSSF SACCOS, Iimefunguliwa Septemba 11, 2024 mbele ya Mh. Bittony Innocent Mwakisu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.


Mshtakiwa ameshtakiwa kwa jumla ya makosa 311 yakiwemo; Kughushi, Kuwasilisha nyaraka zenye taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 333,335(d)(i), 342 na 337 vyote vya Kanuni ya Adhabu, (Sura 16 Rejeo 2022) pamoja na kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa kiasi cha Tshs.338,172,694/= kinyume na kifungu cha 28(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Sura 329 Rejeo 2022).


Uchunguzi umethibitisha kwamba Mshtakiwa alidanganya na kuwezesha kulipwa, huku akijifanya ana ridhaa ya wanachama, mikopo mbalimbali kupitia hundi 144.


Mshtakiwa amekana makosa yote na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa.


Shauri hili ambalo lineendeshwa na Waendesha Mashtaka Hassan Dunia na Gloria Mwainyekule, limeahirishwa hadi Septemba 25, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.