MAANDALIZI YA ONESHO LA S!TE 2024:WAONESHAJI ZAIDI YA 120 KUSHIRIKI JIJINI DAR ES SALAAM.

 


DAR ES SALAAM.

KUELEKEA onesho la Nane la Swahili International Tourism Expo S!TE 2024 imeelezwa kuwa onesho hilo siyo tu litakuza sekta ya utalii na shughuli zake nchini bali pia linatarajiwa kuwaleta pamoja waoneshaji (Exhibitors) wa wa bidhaa na huduma za utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za utalii (International Hosted Buyers) takribani 120 kutoka Nchi ambazo ni masoko ya kimkakati ya utalii wa Tanzania ikiwemo Nchi za Asia, Ulaya, na Amerika.  


Akizungumza na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini,leo Septemba 24, 2024 Makao makuu ya bodi hiyo Jijini Dar Es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru amesema maandalizi ya onesho hilo kubwa na la kimataifa yanaendelea vyema ambapo pia litakalofanyika Oktoba 11 hadi 13 mwaka huu.


Mafuru amewaambia waandishi wa Habari kuwa wadau mbalimbali wanaotarajiwa kushiriki Onesho la S!TE 2024 ni pamoja na Wakala wa Biashara za Utalii (Tour Operators), Watoa Huduma za Malazi (Accommodation Facilities), Wakala wa Safari (Travel Agents), Wakala wa Meli za Watalii (Cruise ship agents)na Waongoza Watalii (Tour Guides)," amesema Mafuru na kuongeza wengine ni,


"Vyama vya Utalii (Tourism Associations), Wajasiriamali wa bidhaa za utalii, Bodi za Utalii (Tourism Boards), Taasisi za Uhifadhi (Conservation Authorities), Taasisi za Kifedha (Financial Institutions), naTaasisi za Elimu za Utalii (Tourism Learning Institutions),amesema  


Mafuru ametaja nchi zilizothibitisha kushiriki hadi sasa kuwa ni China, Denmark, Finland, Japan, Afrika Kusini, Hispania, India, Oman, Urusi, Misri, Uholanzi, Nigeria, Brazil, Ujerumani, Kenya, Ethiopia, Uganda, Lesotho naTanzania.


Kwamba shughuli zitakazofanyika wakati wa S!TE 2024 ni Maonesho ya Utalii (Exhibitions), Mikutano ya Kibiashara (B2B, B2G, B2C, G2G), Semina za masuala ya utalii na masoko (Seminars), Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Utalii (Tourism Investment Forum) na Ziara za Mafunzo za kutembelea vivutio vya utalii (FAM Trips). 

Amesema ziara hizo zitajikita katika Kanda za Utalii Kusini (Southern Circuit), Magharibi (Western Circuit) na Zanzibar kama Gombe National Park and Kigoma City Tour, Mikumi and Udzungwa Mountain National Parks, Ruaha National Park and Iringa Active Safari Fam Trip, Nyerere National Park, Pugu Kazimzumbwi Forest, Dar es Salaam and Kilwa Ruins, Mafia Island, na Zanzibar Fam Trip.


Chimbuko la Onesho la S!TE: Onesho la S!TE (Swahili International Tourism Expo) lilianzishwa mwaka 2014 kwa lengo la kuwakutanisha watoa huduma mbalimbali waliopo katika mnyororo wa thamani wa utalii (Tourism Value Chain) kutoka ndani na nje ya Nchi. 


Aidha, tangu kuanzishwa kwake Onesho la S!TE limeendelea kuimarisha mtandao wa kibiashara (Business Networking) hususan baina ya wafanyabiashara za utalii waliopo Nchini na wenzao kutoka katika Masoko ya Utalii (Source Markets) hivyo, kuchagiza ongezeko la watalii na ukuaji wa Sekta ya Utalii kwa ujumla.  


Kadhalika, Onesho la S!TE limekuwa likitoa fursa ya kutangaza vivuto vya utalii na fursa za uwekezaji. Mwaka huu (2024) ambao ni msimu wa nane (8) wa Onesho la S!TE, litafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.   


Kauli Mbiu ya S!TE 2024: “Explore Tanzania for a Life Time Investment and Seamless Tourism Experience” au “Tembelea Tanzania kwa Uwekezaji Endelevu na Utalii usiomithirika”. 


 Nyenzo zinazoongoza S!TE 2024?:Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999; Mkakati wa Kutangaza Utalii Kimataifa (2020-2025); Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano III (FYDP III 2021/22 – 2025/26); Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 – 2025; na Programu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.     


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.