MAFIA BOXING PROMOTION YAJA NA "KNOCKOUT YA MAMA" KATIKA USIKU WA KIHISTORIA.


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mafia Boxing Promotion Antonio Nugaz akizungumzia na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu,

Dar es salaam.

KAMPUNI ya Mafia Boxing Promotion imetangaza rasmi pambano la kubwa la ngumi la Kimataifa "Knockout ya Mama" litakalofanyika Oktoba 5, 2024 katika ukumbi wa Magomeni City Centre (soko la magomeni)jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 26, 2024 jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Antonio Nugaz amesema kwamba pambano hilo litawakutanisha mabondia Ibrahim Mafia Tz na Said Chino katika kuwania mkanada wa WBC.


“Kama ilivyo katika Mchezo wa Mpira wa miguu,Rais Dkt Samia amekua akitoa zawadi ya fedha kwa kila Gori linalofungwa katika mechi za Kimataifa ili kuleta motisha kwa wachezaji,nasisi huku atujakaa mbali tumeamua kuja na pambano hili ( Nock out ya Mama) mshindi atapata milioni kumi kama bonasi” amesema Nugaz.


Ameogeza kuwa pambano hilo la Kimataifa lina lengo la kuwafanya mabondia wa kitanzania kupigana Kimataifa zaidi ili kuweza kufikia Malengo yao katika Mchezo huo.


Nugaz amesema kwamba mgeni rasmi katika pambano hilo atatangazwa hivi karibuni,nakubainisha kuwa viingilio ni elfu kumi( 10000,) elfu thelathini( 30000,) na elfu hamsini(50000).


Wakizungumza kwa nyakati tofauti mabondia hao wamesema kuwa wapo tayari kupambana katika pambano hilo nakwamba mashabiki wa mchezo wa ngumi watarajie burudani ya aina yake.


Bondia Ibrahim Mafia Tz amesema kwamba amejiandaa na anaendelea kujiandaa vizuri ili aweze kushinda pambano hilo.


“Mashabiki wasiwe na wasiwsi ,nipo vizuri nawakaribisha wajitokeze kwa wingi kuja kushuhudia pambano siku hiyo” amesema.


Naye bondia Said Chino amesema kuwa yupo tayari kupigana kwenye pambano hilo nakwamba kwa sasa anaendelea kujifua ili kuweza kumshinda mpinzani wake.

“Nimejiandaa vizuri kazi itaonekana naamini hivo,mashabiki watapata burudani ya kutosha na pia nitashinda pambano hilo” amejigamba Chino mbele ya Waandishi wa habari.




Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.