Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim James Yonazi amewasihi Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Kufanya kazi kwa karibu na Idara ya Menejimenti ya Maafa iliyopo Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuweza kuratibu programu za uokozi kwa majanga ya majini na usalama wa bahari kwa ujumla.
"Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu shirikianeni na Taasisi nyingine za kisekta na kuwa na mpango mkakati wa matumizi ya boti hii katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu majini".
Hayo ameyasema leo September 19/2024 wakati wa Hafla ya makabidhiano ya Boti ya Doria (PB Sailfish) kati ya ofisi ya Waziri Mkuu na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ambapo amesema Serikali inataka kuona boti hiyo inatumika ipasavyo katika shughuli zilizopangwa na zitakazojitokeza kwa mujibu wa mahitaji ya matumizi kwa wakati husika. Aidha, naomba kuwasisitizia kuwa matumizi ya boti hii pia yazingatie Mwongozo wa Kitaifa wa Kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu wa mwaka 2022.
Ameongeza kuwa Lengo kuu la kununuliwa kwa boti hii ni kuimarisha doria ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu nchini. Doria hizo ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukabialiana na vitendo vya kihalifu kama vile uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishaji wa dawa za kulevya, biashara za magendo na utoroshwaji wa nyara za Serikali. Hivyo, ni matumaini yangu kuwa boti hii itatimiza lengo hilo na kuimarisha juhudi za Serikali za kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika eneo letu la bahari.
"Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ina imani kubwa na uwezo wa TASAC katika usimamizi, uendeshaji na utunzaji wa boti hii. Hiyo ndiyo sababu iliyopelekea boti hii kukabidhiwa kwa Shirika hili. Ni imani yetu kuwa mtaitunza vizuri boti hii ikiwa ni pamoja na kuifanyia matengenezo kinga kwa wakati na hivyo kuwaongezea ufanisi katika kazi zenu za kila siku hususani katika ukaguzi kwa meli zinazoingia kwenye maji yetu ya ndani".
Amebainisha kuwa TASAC ilishirikiana kwa karibubna ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutoa ushauri na kushiriki katika kutengenezwa kwakembapo boti hiyo itakuwa xhachu a kuongeza usala baharini,kuhifadhi mazingira kwa kudhibiti umwagaji wa mafuta baharini,
Pia amehidi kukitumia vema chombo hicho kwa kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za baharini wakiwa salama na wanaofwata sheria za usalama baharini bila shuruti.
Kupatikana kwa boti hiyo kutasaidia kuimarisha ulinzi na kupambana na vitendo vya uharifu wa uporaji waboti,usafishaji haramu wa binadamu na bidhaa mbalimbali, katika mwambao wa Bahari na Maziwa Makuu.
Hakuna maoni: