VIONGOZI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WATAKIWA KUWAJIBIKA KUKOMESHA VITENDO VYA MAUJIA NA UKATILI NCHINI.


DAR ES SALAAM.

Viongozi na vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa wanapaswa kuwajibika kwa matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu, na kuchukua hatua za haraka na za makusudi kukomesha vitendo hivyo bila kungojea msukumo.

Akizingumza na Waandishi wa Habari Mapema Leo September 10/2024 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku,ambapo amesema kuwa viongozi hao hawapaswi kudai hawajui waathirika na wahusika wa vitendo hivyo badala yake wawajibuke kulingana na matakwa ya majukumu yao ya kazi ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

"Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue. Kwahiyo Taasisi ya Mwalimu Nyerere inaomba tumsaidie Rais kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hao ili achukue hatua stahili. Anavyo vyombo vya dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpa taarifa za uhakika.Viongozi wa vyombo hivi wasituambie kwamba hawajui, wanajua. Wasituambie kwamba wanamuogopa Rais, wasimsingizie". Amesema Butiku na kuongeza kuwa 

"Rais amewateua kwa madhumuni ya kulinda usalama wa nchi na mali zake, na kwa hivyo wanapaswa kuchukua hatua bila kusubiri maelekezo. Rais hawezi kuondoa kila mtu anayehusika; viongozi hawa wanajua kinachoendelea,".

Aidha Butiku amewataka Watanzania wote na kuwaomba kushirikiana kumuunga mkono kwa dhati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kukomesha tabia mbaya zilizozuka katika Taifa za kulawiti, kuteka, kunyanyasa na kuua Watu.

"Tunaye Rais mmoja tu sio wawili wala watatu tuliye mkabidhi Katiba ya nchi yetu ili aitumie kuongoza Taifa letu na kulinda na kuhakikisha usalama wa Watanzania wote na wageni halali wanaoingia katika Taifa letu, na pia kulinda mali zetu. Huu ni wajibu wa Kikatiba wa Rais wetu anautekeleza kwaniaba yetu tumuunge mkono bila maswali"Amesema Butiku.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.