VITONGOJI 15 KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA REA WILAYANI MAGU.



 

Magu- Mwanza 

Vitongoji 15 katika Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza vinatarajiwa kunufaika na mradi wa Kusambaza umeme kwenye vitongoji 135 Mkoani Mwanza unaotekelezwa *na* Wakala wa Nishati Vijijini ( REA).


Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa mradi wa Wakala wa nishati vijijini (REA) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Awesa Mnunduma wakati wa kumtambulisha Mkandarasi atakayetekeleza mradi huo , Ceylex Engineering (pvt) Limited kwa Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari .


Akizungumza wakati akimtambulisha Mkandarasi huyo katika ofisi ya mkuu wa Wilaya leo Jumatano Septemba 25, 2024 Mhandisi Mnunduma amesema kuwa jumla ya vitongoji 135 vya mkoa wa Mwanza vitanufaika na mradi huo ambapo kwa Wilaya ya Magu vitongoji 15 vitanufaika na mradi.


Amesema kila jimbo katika majimbo 9 ndani ya mkoa wa Mwanza vitongoji 15 vitasambaziwa umeme kupitia mradi huu wenye thamani ya shilingi Bilioni 19.38 ( 19,389,153,096.05) 


Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi Bilioni 19 kutekeleza mradi huo.


Aidha amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha kwa muda uliopangwa ili kuepuka changamoto ya baadhi ya wakandarasi kushinda kukamilisha miradi ya Serikali kwa wakati.


Naye Mkandarasi anayetekeza mradi huo alimuhakikishia DC Nassari kuwa atatekeleza mradi kwa mujibu wa mkataba na kwamba maandalizi yote muhimu amekwishafanya.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.