Michael Smith, mwanamuziki mwenye umri wa miaka 52 kutoka North Carolina, Marekani ameshtakiwa kwa kesi ya ulaghai wa kipekee inayohusisha akili Mnemba (Akili Bandia), maarufu kwa jina la AI.
Kama ilivyoandikwa na jarida la *Blue Tech Wave*, mpango wa Smith unawakilisha tukio la kwanza linalojulikana la kuongeza idadi ya wasikilizaji bandia wa nyimbo ili kujivunia kipato.
Mamlaka za serikali nchini marekani zinadai kuwa Smith aliajiri akili bandia kuzalisha mamia ya maelfu ya nyimbo mbalimbali, ambazo si halisi, na kuunda mkusanyiko mkubwa wa nyimbo hizo katika muundo wa Playlist
Ili kutengeneza pesa zaidi, alitumia akaunti bandia (bOT) kama yale ya telegram kuonyesha nyimbo, zikichezwa (play) kwa kurudiwa (on repeat) na kusikilizwa mara nyingi, ambazo zimekuwa zikikusanya malipo ya kifisadi kwenye majukwaa ya mtandaoni.
Operesheni ya Smith ilianza muda mrefu, na ilikua kubwa hadi kufikia hatua ya kuripotiwa, alifanikiwa kuzalisha zaidi ya dola milioni 10 (sawa na Tshs. Bilioni 250) kutoka kwenye malipo ya kifisadi.
Katika barua pepe zilizotajwa kwenye hati ya mashtaka, Smith alielezea mkakati wake wa kukwepa hatua za kuzuia udanganyifu, akisema, “Tunahitaji kupata idadi KUBWA ya nyimbo haraka ili kufanikisha ujanja huu dhidi ya sera za kuzuia udanganyifu wanazotumia sasa.”
Smith alibadilisha mfumo huo ili kujipatia faida kubwa kifedha, akidhoofisha kwa kiasi kikubwa uadilifu wa tasnia ya muziki na kuvuruga mapato kutoka kwa wasanii halali na hakimiliki.
Mkurugenzi msaidizi wa muda wa FBI, ndugu Christie M. Curtis, alibainisha uzito wa kesi hiyo, akisema, "Mpango wa mshtakiwa ulilenga uadilifu wa tasnia ya muziki kwa jaribio la makusudi la kukwepa sera za majukwaa ya utiririshaji (streaming)"
Hakuna maoni: