BAADHI ya Watumishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wameshiriki Kongamano la tatu la ufuatialiaji na tathimini unaofanyika Zanzibar na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali.
Mbali na watumishi hao, pia walengwa na wanufaika wa mfuko huo walishiriki maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano hilo.
Akizungumza jana, Mtaalam wa masuala ya TEHAMA wa Mfuko huo, Peter Lwanda, alisema lengo la kushirki katika mkutano huo ni kujifunza na kuongeza ujuzi kwenye suala zima la kufanya tathimini na ufuatiliaji.
"Kitengo kama hiki sisi TASAF tunacho muda mrefu, lakini kwa sababu tunafanya Ufuatiliaji na kufanya tathimini kwenye kiradi yetu mbalimbali, mkutano huu ni muhimu kwetu kuongeza ujuzi na kuendelea kujifunza ili kuwa na uhakika wa kufanya kazi kwa ufasaha," alisema Lwanda.
Aidha, aliweka wazi TASAF wamekuwa wakiendesha miradi mbalimbali Zanzibar na katika mkutano huo pia walifanya maonyesho mafanikio yaliyofikiwa na walengwa wa mfuko huo visiwani Zanzibar.
"Lakini kwenye suala la tathimini, sisi pia tumekuwa tukijitathimini kwa kutumia wataalam kutoka nje ya TASAF tukiamini hatuwezi kujitathimin wenyewe kama tunataka matokeo sahihi, na kikubwa ni kuhakikisha malengo ya mfuko huu yafakiwa katika kila miradi yake," alisema.
Mkutano huo wa tatu ulioanza Septemba 17 na kushirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali, unamalizika leo visiwani humo.
Hakuna maoni: