Dar es salaam,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi, atatembelea ofisi za Chama cha National League for Democracy (NLD) zilizopo Tandika Magorofani jijini Dar es Salaam, tarehe 8, Oktoba 2024.
Katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ataambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mtungi. Mhe. Lukuvi, atakutana na Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Mhe. Mfaume Khamis, na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo.
Aidha Mhe. Lukuvi ataangazia masuala mbalimbali katika ziara hiyo, yenye lengo la kufahamiana, kusalimiana na kuzungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye usajili kamili.
Hakuna maoni: