WAANDISHI WA HABARI WAPEWA ELIMU KUHUSU MPOX, MARBURG.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Afya imewatoa mafunzo kwa waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu ugonjwa tishio wa Mpox na Marburg, huku ikiwataka wananchi kutumia namba 199 kutoa taarifa pale wanapoona dalili za magonjwa hayo.

Aidha Wizara ya Afya imesema katika kukabiliana na magonjwa hayo imeelekeza nguvu katika mikoa 14 ambayo inapokea wageni kwa asilimia kubwa nchini.

Mafunzo hayo yametolewa Oktoba 4,2024 katika Ukumbi wa CTC Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ambapo lengo ni kuhakikisha kundi hilo linakuwa na uelewa kuhusu magonjwa hayo ambayo hayana tiba ya moja kwa moja.


Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Dkt.Ona Machangu amewataka wanahabari na wahariri kutumia kalamu zao kuweza kufikishia jamii elimu juu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

"Wanahabari na wahariri wote tuelimishe na kuhamasisha jamii kuweza kufuata hatua mbalimbali za kujikinga kama kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kuepuka kushikana mikono",amesema Dkt.Ona

Dkt.Ona ameishauri jamii kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari ili kujikinga na magonjwa hayo kwani tayari nchi jirani zina maambukizi ya magonjwa hayo.

Kaimu mkurugenzi huyo amesema elimu pekee ndio njia muafaka kwa jamii kukabiliana na magonjwa hayo ya milipuko, hivyo waandishi ni kiungo muhimu kutoa elimu hiyo.

Aidha Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini katika Wizara ya Afya Englibert Kayombo amesema semina hiyo ya waandishi wa habari ni endelevu na taratibu za wizara kukaa pamoja na wadau hao ili kuwapa elimu muhimu itakayosaidia kutoa taarifa kwa usahihi.

Kayombo amesema Wizara itahakikisha elimu inatolewa kuhusu magonjwa hayo na mengine ili kuifanya nchi na wananchi wawe salama.

Naye Mratibu wa Kitaifa, Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Dk Norman Kyala amesema katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko serikali imeweka mkazo katika maeneo yote ambayo yanaruhusu mwingiliano.

"Katika kukabiliana na haya magonjwa ya Marbug na Mpox tumeweka kipaumbele katika mikoa 14, ikiwemo Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Dodoma, Mbaya, Songwe, Shinyanga na mingine," amesema.

Dk Kyala amesema magonjwa hayo yanaambukizwa kupitia majimaji, damu, vitu vyenye ncha kali, mate, kujamiana na njia nyingine, hivyo kuitaka jamii kuwa makini na kutoa taarifa pindi wanapoona dalili.

Mratibu wa Mafunzo James Mhilu amewata waandishi wa habari na wahariri kuwakumbusha wananchi kupiga namba 199 kituo cha miito ya simu cha Wizara ya Afya kwa taarifa, maoni na ushauri.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.