DAR ES SALAAM.
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imejipanga kuchukua hatua kali dhidi ya wapangaji wanaoshindwa kulipa kodi ya pango kwa wakati, kwani Hali hiyo inakwamisha mipango ya maendeleo na ukarabati wa nyumba.
Akizingumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Oktoba 02/2024 Mtendaji Mkuu wa TBA, ARCH Daud Kondoro, Amesema kuna malimbikizo ya madeni yanayokaribia shilingi bilioni 14.8. huku Wapangaji 648 tayari wamepewa notisi za kulipa, huku zoezi la kuwaondoa likitarajiwa kuanza Oktoba 7, 2024, likiratibiwa na dalali wa Mahakama, Twins Action Mart.
Arch Kondoro amesisitiza kuwa hatua za kisheria zitaxhukuliwa dhidi ya wapangaji hao wakaidi, ikiwa ni pamoja na kuwafungulia kesi za madai. TBA pia inatekeleza mfumo wa kielektroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) ili kuboresha ukusanyaji wa kodi.
Aidha, mpangaji anayeishi kwenye nyumba za TBA atakuwa na fursa ya kulipwa kodi moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wake, huku vitasa janja na smart meters vikiendelea kufungwa kwenye majengo yote mapya.
Arch Kondoro alihimiza wapangaji kulipa madeni yao kwa wakati ili kusaidia juhudi za ujenzi wa makazi bora, na aliwataka wananchi kufuatilia taarifa za TBA kupitia mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya wakala.
Hakuna maoni: