UTT AMIS YAWAHAKIKISHIA WATANZANIA UWEKEZAJI SALAMA NA FAIDA BORA.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App
Na Emmanuel Kawau,
Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya UTT Asset Management and Investment Services (UTT AMIS), Prof. Faustine Kamuzora, amesema kuwa uwekezaji katika mifuko ya UTT ni njia salama na rahisi kwa Watanzania kujiwekea utulivu wa kifedha. 

Ameyasema hayo wakati akizingumza na Waandishi wa Habari November 15,2024 kabla ya kuanza kwa
Mkutano Mkuu wa Wawekezaji wa Mfuko wa Umoja (Umoja Fund) jijini Dar es Salaam, Prof. Kamuzora amesisitiza kuwa uwekezaji huo unawapa watu fursa ya kupata faida bila ya kuwa na wasiwasi wala kutumia nguvu kubwa katika kushughulikia fedha zao kila wakati.
Published from Blogger Prime Android App
Prof. Kamuzora alisisitiza umuhimu wa kuwekeza, akisema, “Kikubwa ni kuwekeza, bila kuwekeza huwezi kutajirika.” Aliongeza kuwa mifuko ya UTT ni salama na inafaa kwa mtu yeyote, kwa sababu inatoa fursa ya kuwekeza kwa viwango vidogo na pia inatoa faida nzuri kwa muda mrefu. Alisema kuwa elimu ya fedha inahitajika kwa kila Mtanzania ili kuwaondoa katika umaskini na kuwasaidia kutambua umuhimu wa kuwekeza na kuendesha maisha bora.

“Mifuko yote sita inayosimamiwa na UTT AMIS imekuwa na mafanikio makubwa, na faida ya uwekezaji katika mifuko hii inapatikana kila mwaka,” alisema Prof. Kamuzora. Alieleza kuwa mifuko ya UTT ni bora kwa mtu yeyote anayehitaji njia rahisi ya kuongeza kipato bila ya kuwa na wasiwasi wa kudhibiti uwekezaji wake kila wakati.

Published from Blogger Prime Android App
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, amesema kuwa UTT AMIS imeendelea kufanya vizuri katika mwaka huu wa fedha ambapo thamani ya mifuko hiyo imeongezeka kutoka Shilingi Trilioni 1.5354 hadi Shilingi Trilioni 2.2382 hadi kufikia Juni 30, 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 45.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Migangala alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na faida iliyopatikana katika uwekezaji na ongezeko la idadi ya wawekezaji, ambapo 79,519 wamejiunga na mifuko ya UTT mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 32 kutoka 47,480 mwaka 2023.

Migangala ameongeza kuwa mwaka huu wameweza kuvuka malengo yao, na kwamba wameweka lengo la kufikia Shilingi Trilioni 2.5 ifikapo mwaka 2025. Alifafanua kuwa mwaka huu wameweza kufikia kiwango cha Shilingi Trilioni 2, licha ya kuwa lengo lilikuwa kufikia kiwango hicho mwaka 2025.
Published from Blogger Prime Android App
Mkurugenzi huyo ameeleza pia kuwa wanaendelea na juhudi za kuboresha mifumo ya teknolojia na huduma zake za uendeshaji ili kuwapa wawekezaji huduma bora zaidi na faida zaidi kadri soko la mitaji linavyokua. Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wawekezaji wanapata faida nzuri na kwamba UTT AMIS itaendelea kuboresha mifumo yake ya kiteknolojia ili iwe rahisi kwa watu kufungua akaunti na kufanya uwekezaji kupitia mtandao.

“Tunataka kuwasaidia Watanzania kufikia malengo yao ya kifedha kwa kuwekeza katika mifuko ya UTT, na tunawaahidi wawekezaji wetu kuwa mifuko hii ni salama na inatoa faida bora,” alisema Migangala.

Kwa ujumla, Mkutano Mkuu wa Wawekezaji wa Mfuko wa Umoja ulionyesha mafanikio ya mifuko yote sita inayosimamiwa na UTT AMIS, ambayo ina thamani inayokua kwa kasi na kutoa faida kwa wawekezaji wake. UTT AMIS imejizatiti kuhakikisha kuwa huduma zake zinaendelea kuboreshwa ili kutimiza malengo yake ya kusaidia Watanzania kuwekeza na kuwa na mustakabali bora wa kifedha.



Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.