DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema zoezi la uokoaji halijasimama kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, ukweli ni kwamba zoezi linaendelea hakuna kilichosimama ndio maana viongozi mbalimbali wapo hapo kuhakikisha zoezi hilo linaendelea.
Aidha toka uokoaji uanze hadi kufikia saa 11:00 jioni watu 70 wameokolewa wakiwa hai lakini kwa mujibu wa taarifa za kidaktari watu 4 tu ndio wamepoteza maisha.
Sanjari na hilo RC Chalamila amevishukuru vikosi mbalimbali na wadau wingine ambao wanaendelea kutoa misaada ya hali na mali ili kufanikisha shughuli nzima ya uokozi.
Vilievile amesama taarifa kwa umma itaendelea kutolewa kadri zoezi hilo linavyoendelea aidha ifikapo saa 4:30 usiku atatoa tena taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya uokoaji.
Hakuna maoni: