DAR ES SALAAM.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 18, 2024 amekagua muendelezo wa zoezi la uokoaji katika jengo lililodondoka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam na amesisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi atakapotolewa mtu wa mwisho aliyekwama kwenye jengo hilo.
Aidha Majaliwa amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamtafuta mmiliki wa jengo hilo ili aweze kusaidia kufahamu juu ya chanzo cha kudondoka kwa jengo hilo.
Pia ametoa wito wa watanzania kuacha kuchangisha kiholela kwani Serikali inaoutaratibu wa utoaji wa misaada kupitia Kamati ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hakuna maoni: