DAR ES SALAAM.
Airtel Tanzania imeanza msimu wa sikukuu kwa kishindo kupitia kampeni kabambe ya Airtel Santa Mizawadi, yenye lengo la kuwashukuru wateja na mawakala wake waaminifu kwa kuendelea kutumia huduma za Airtel. Promosheni hii maalum itatoa zawadi kemkem zikiwemo pocket WIFI, simu janja, pikipiki, runinga za Smart TV (inchi 75), na pesa taslimu hadi shilingi milioni moja.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando, promosheni hii inalenga kuleta furaha na kuonesha upendo kwa wateja na mawakala katika msimu huu wa sikukuu. "Kupitia Airtel Santa Mizawadi, tunanogesha msimu wa sikukuu kwa wateja wetu na mawakala wanaoendelea kuwa nasi katika safari ya mafanikio," alisema Mmbando wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika Desemba 17, 2024, jijini Dar es Salaam.
Ili kushiriki na kushinda zawadi za Airtel Santa Mizawadi kwa Mawakala: Fanya miamala ya kuweka na kutoa fedha kupitia huduma za Airtel. Huku kwa Wateja wanapaswa kufanya miamala kama vile kununua bando, kutuma au kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa kimataifa, au kununua vifurushi kupitia 14999#, 15060#, au kwa kutumia My Airtel App.
Washindi wa promosheni hii watapatikana kupitia droo zitakazochezeshwa kila wiki. Airtel imesisitiza kuwa washindi wote watapigiwa simu kupitia namba yao rasmi ya huduma kwa wateja, 100.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Bi. Celine Njuju, alibainisha kuwa Airtel imeleta promosheni hii ili kuthamini mchango wa wateja na mawakala wake. Aliwaahidi wateja kuwa watapata fursa ya kukutana na Mr. Santa wa Airtel, ambaye atazunguka mitaani kutoa zawadi za papo kwa hapo.
"Ukikutana na Mr. Santa wetu, utaona jinsi Airtel inavyothamini wateja na mawakala wake. Atanogesha msimu wako wa sikukuu ili ufurahie wewe na familia yako," alisema Bi. Njuju.
Airtel inawahimiza wateja na mawakala wake kutembelea tovuti yao au kuwasiliana na huduma kwa wateja kupitia namba 100 kwa maelezo zaidi kuhusu promosheni hii kabambe.
Furahia msimu wa sikukuu na Airtel Santa Mizawadi!


Hakuna maoni: