DKT. BITEKO ASEMA SERIKALI ITAKULA SAHANI MOJA NA WANYANYASAJI WA WENYE ULEMAVU.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Serikali haitavumilia wala kupuuza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu, na itachukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Published from Blogger Prime Android App
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Biteko alisema kwamba wale wanaojihusisha na vitendo vya unyanyasaji, kama vile kuuza viungo vya albino au kufanya mauaji, watachukuliwa hatua kali. Aliyekuwa akimwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, alisisitiza kuwa Serikali inataka kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinaheshimiwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Katika mkutano huo, Mhe. Biteko alizindua Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi wa Watu Wenye Ualbino pamoja na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi kwa Wenye Ulemavu. Alitoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia miongozo ya Serikali, ikiwemo kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa saidizi na kuhakikisha utekelezaji wa mikakati hiyo unakuwa wa kweli na endelevu.

Published from Blogger Prime Android App
Aidha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwan Kikwete, alisisitiza umuhimu wa jamii kutambua haki za kijamii za watu wenye ulemavu, huku akiongeza kuwa mkakati huo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya watu hao.

Mkutano huo pia ulijumuisha shukrani kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mhe. Riziki Lulida, kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuwawezesha watu wenye ulemavu katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.