SERIKALI YAWEKEZA ZAIDI YA BILION 222 KUENDELEZA SAYANSI NA UBUNIFU.

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema tangu mwaka 2015, Serikali ya Tanzania imeweka juhudi katika kuendeleza sekta ya sayansi, teknolojia, na ubunifu kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 222.8, ili kujenga uwezo wa watafiti na wabunifu wa ndani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho jijini Dar es Salaam, Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu wa kutambua na kuthamini michango ya wanasayansi na wabunifu wa ndani, akisema kwamba tafiti zao zinapaswa kutumika kutatua changamoto za kijamii badala ya kutambuliwa zaidi nje ya nchi.

Amesema, "Tafiti za wanasayansi wetu zinapaswa kutumika katika kutatua matatizo yetu, na kila anayejaribu kufanya utafiti apewe fursa, ili aendelee na kazi yake na matokeo yake tutayaona," na kuongeza kuwa Serikali kupitia COSTECH imetoa kiasi cha bilioni 32 kwa ajili ya miradi ya utafiti na ubunifu.

Aidha, Dkt. Biteko pia amezindua rasmi mfuko wa mikopo nafuu wa "SAMIA FUND" ambao utasaidia kuhamasisha biashara zinazotokana na tafiti na ubunifu nchini. Mfuko huu unatarajiwa kusaidia watafiti na wabunifu kupata mitaji nafuu ili kuboresha na kuendeleza miradi yao.

Published from Blogger Prime Android App
Kwa upande mwingine, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali inatambua juhudi za wanasayansi wa ndani, na baadhi yao tayari wametunukiwa vyeti kwa kutambua mchango wao katika maendeleo, hasa katika sekta za afya, kilimo, na uvuvi. Aliongeza kuwa hatua hizi ni sehemu ya kuhakikisha jitihada za wanasayansi na watafiti wa ndani zinaendelea kuwa na manufaa kwa taifa.

Published from Blogger Prime Android App
Nae Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na msaada inayoitoa, akieleza kuwa COSTECH imeweza kufanikisha kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kuwa moja ya taasisi zinazoongoza Kusini mwa Jangwa la Sahara. Dkt. Nungu pia alibainisha kuwa COSTECH imeweza kutoa vibali 1000 kwa watafiti kutoka nje ya nchi, jambo ambalo limewezesha kubadilisha ndoto za vijana wengi kuwa fursa.

Balozi wa Norway nchini, Mhe. Tine Tonnes, alipotolea mfano juhudi za Tanzania katika kuendeleza utafiti na ubunifu, alisema kuwa nchi yake itaendelea kutoa msaada kwa Tanzania, hasa katika miradi inayohusiana na uhifadhi wa mazingira.

Katika kongamano hilo, vikundi 19 vilivyotekeleza tafiti na ubunifu zilizozalisha matokeo chanya walipokea mfano wa hundi ya shilingi bilioni 6.3 kama mkopo kwa ajili ya kuendeleza miradi yao. Hii ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa tafiti na ubunifu vinakuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa maendeleo ya nchi.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.