WAHADHIRI NA WANAFUNZI VETA WAJA NA BUNIFU KABAMBE KATIKA KONGAMANO LA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU.
Kongamano la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC), lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTEC) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Chuo cha VETA Chang'ombe kimetumia kongamano hilo kuonesha bunifu mbalimbali kizinazobuniwa na wanafunzi na wahadhiri wake. Miongoni mwa bunifu hizo ni dawa za kutibu fangasi na UTI, dawa za kuzuia malaria kwa kutumia mbu, pamoja na kifaa cha kufundishia mfumo wa jua na Atomu.

Akizungumza kuhusu kongamano hilo, Meneja wa Uhusiano kwa Umma wa VETA Chang'ombe, Sitta Peter, amesema kwamba kongamano hilo linadumu kwa siku tatu na ni jukwaa la kuonyesha bunifu mbalimbali zinazobuniwa na wanafunzi na wahadhiri wa VETA. Alisisitiza umuhimu wa Watanzania kutumia bunifu zinazotolewa na wenzao ili kuhamasisha ubunifu zaidi na kuboresha maisha ya watu katika jamii. Peter pia alieleza kuwa maonesho hayo yatatumika kuonyesha jinsi bunifu zinavyoweza kutatua changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii, huku akiwataka Watanzania kuongeza ufanisi katika kubuni bidhaa zitakazosaidia kutatua matatizo yao.
Kwa kipindi cha miaka mitano, VETA imefanikiwa kuibua bunifu 118, ambapo 13 zimefanikiwa kuingia sokoni, huku 45 nyingine zikikamilisha mchakato wa kuingizwa sokoni. Huu ni ushahidi wa juhudi kubwa zinazofanywa na taasisi hiyo katika kukuza ubunifu na kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi kwa kutumia sayansi na teknolojia.
Alli Issa, Mwalimu wa VETA Dar es Salaam, alisema kuwa baadhi ya bunifu tayari zimepata hati miliki ili kuhakikisha kuwa ufanisi wa kazi hizo hautaingiliwa na watu wengine. Aliongeza kuwa bunifu ambazo bado hazijaingia sokoni, wanazidi kufuata mchakato wa kupata miliki ili zitakapofanikiwa ziweze kuingizwa kwenye soko la ndani na nje. "Kuwa na miliki ya bunifu ni jambo la muhimu sana kwa wabunifu wetu ili kulinda haki zao na kuzuia matumizi yasiyofaa," alisema Issa.
Mvumbuzi wa kifaa cha kufundishia mfumo wa jua na Atomu, Ernest Malanya, alieleza furaha yake kwamba kifaa chake kilipata ithibati kutoka Wizara ya Elimu kwa ajili ya kufundishia katika shule za msingi na sekondari. Malanya ambaye pia ni mwanafunzi wa VETA, alieleza kuwa kifaa hicho kinasaidia wanafunzi kuelewa vyema muktadha wa masomo ya sayansi, hasa somo la jua, ambalo limekuwa na changamoto kubwa katika ufundishaji na ufahamu. "Nina imani kuwa kifaa hiki kitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo vifaa vya kufundishia ni vichache," alisema Malanya.
Malanya alitoa wito kwa Serikali na wadau wa elimu kumsaidia kwa mtaji ili kuongeza uzalishaji wa kifaa hicho kwa wingi, ili kufikia shule nyingi zaidi nchini. "Kutengeneza kifaa hiki kwa wingi kutasaidia kuwafikia wanafunzi wengi na kuwaongezea maarifa katika sayansi ya jua, jambo linalosaidia kujenga jamii yenye uelewa wa kisayansi," alisema.
Kongamano hili linatoa jukwaa muhimu kwa VETA na wanazuoni wake kuonyesha mafanikio yao katika matumizi ya sayansi na teknolojia, na linahamasisha jamii kutumia ubunifu wa ndani kutatua changamoto zinazozikumba. Hii ni fursa ya kuonyesha ufanisi wa VETA katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii na sekta mbalimbali za maendeleo.

Hakuna maoni: