DIWANI KIMAMBO ACHANGIA LAKI TANO KWA AJILI YA WASANII KIGAMBONI







MHE. ELIZABETH KIMAMBO, DIWANI VITI MAALUM MANISPAA YA KIGAMBONI, ACHANGIA TSH 500,000 KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WASANII KIGAMBONI


Tarehe 15 Juni 2025, Chama cha Waigizaji Wilaya ya Kigamboni kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi Kata ya Pembamnazi waliandaa Bonanza la Michezo Mbalimbali lenye lengo la kukuza mshikamano, upendo na umoja kati ya wasanii na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Michezo mbalimbali iliyofanyika katika bonanza hilo ni pamoja na kukimbiza kuku, kuvuta kamba, na mpira wa miguu, ambavyo viliwakutanisha vijana, viongozi na wadau mbalimbali kupitia burudani na mazungumzo ya kimaendeleo.


Bonanza hili lilidhaminiwa na Ndg. Abubakari Ally Abubakari, Mkurugenzi wa Boka Pharmacy na City College, kama sehemu ya mchango wake katika kukuza sanaa, michezo na mshikamano wa kijamii Kigamboni.


Mgeni rasmi wa bonanza alikuwa Mhe. Ramadhan Yamlinga, Diwani wa Kata ya Pembamnazi, huku Mgeni Maalum akiwa Mhe. Elizabeth Kimambo, Diwani wa Viti Maalum, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, ambaye aliahidi kuchangia Tsh 500,000 kuunga mkono Tuzo za Kigamboni Awards zinazotarajiwa kufanyika tarehe 6 Julai 2025.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.