Na Damari Tandasi
MKUU wa Kitengo Cha Mafunzo kwa wateja wakubwa na Serikali Anatori lelo amewaasa wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo mbalimbali wanaotembelea maonesho ya Utalii maarufu kama Karibu Kill Fair ili kupata huduma mbalimbali zikiwemo za kimtandao Kutoka kampuni ya Mawasiliano Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Juni 6,2025 kwenye maonesho hayo yanayofanyika eneo la Viwanja vya Magereza Kisongo jijini Arusha Lelo amesema,wao kama YAS wameshiriki maonesho hayo Ili waweze kutoa huduma mbalimbali za kimtandao kwa wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.
"Tumekujankushiriki kwenye maonesho ya Kill Fair kwa sababu yanawaleta pamoja washiriki wengi hasa Kutoka sekta ya utalii ambapo na sisi YAS tupo kwenye mnyororo huo wa thamani kwa kusapoti utalii kupitia mtandao wetu."amesema Lelo.
Ameongeza kuwa "Sisi tunatoa huduma nyingi katika hoteli,Makampuni katika 'connectivity na mawasiliano,kwa hiyo tumeamua kuja kushiriki kukutana na wateja wetu ."
ameongeza kuwa katika maonesho hayo wanaelimisha jamii kuhusu matumizi ya mtandao hasa wa YAS lakini pia kutatua changamoto za kimtandao zinazowakabili wananchi.
Amesema wameendelea kuboresha mtandao huo haswa kwenye upande wa Intaneti vifurushi vya malipo ya kabla na wakati
Hakuna maoni: