GUITEN, AFRIKA KUSINI.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Urban Mwegelo (@jokatemwegelo), ameweka historia kwa kuwasilisha mapendekezo muhimu kwa niaba ya vijana wa vyama vya ukombozi Kusini mwa Afrika katika Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika mjini Guten, Afrika Kusini.
Miongoni mwa mapendekezo makuu aliyowasilisha ni kuanzishwa kwa Tamasha Kubwa la Vijana wa Vyama vya Ukombozi (Liberations Movement Youth Festival), ambalo litawakutanisha vijana kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Namibia kwa ajili ya mijadala, kubadilishana uzoefu, pamoja na fursa za kiuchumi. Pendekezo hilo limekubaliwa rasmi na viongozi wa vyama hivyo.
Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha Marais wa nchi hizo pamoja na viongozi wa vyama, Jokate alisema:
“Nawashukuru sana viongozi wenzangu wa vyama vya ukombozi kwa heshima kubwa ya kunichagua kuwawakilisha vijana wa vyama vyote vya ukombozi Kusini mwa Afrika kuwasilisha mapendekezo ya vijana. Ni heshima kubwa kuzungumza mbele ya wanamajumui wa heshima na wageni kutoka mataifa mengine nje ya Afrika
Mbali na pendekezo la tamasha, Jokate pia aliwasilisha hoja kuhusu utekelezaji wa sera za kina za vijana ili kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora, mafunzo ya ufundi stadi, ushauri, ajira, fursa za kiuchumi na njia za uongozi kwa vijana katika nchi za ukombozi.
Jokate, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, alishiriki mkutano huo kwa niaba ya vijana wa vyama sita rafiki vya ukombozi: CCM (Tanzania), ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), ZANU-PF (Zimbabwe), MPLA (Angola), na SWAPO (Namibia). Mkutano huo uliandaliwa na ANC chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Comrade Fikile Mbalula na kuongozwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, huku Tanzania ikiwakilishwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkutano huo umefanyika kuanzia Julai 25 hadi Julai 28, 2025.
#uvccm #jokate #tamashalavijana #afrikakusini #vyamavyaukombozi #liberationmovement #ccm #frelimo #anc #zanu_pf #swapo #mpla #afrika2025 #vijanawakomavu #uchumiwavijana
Hakuna maoni: