MIRIAM ODEMBA ATOA WITO WA KUCHANGIA UJENZI WA VYOO SHULE YA MSINGI MWENDAPOLE


PWANI.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation (MOF), ambaye pia ni mwanamitindo nguli wa kimataifa, Miriam Odemba, amesisitiza Watanzania kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyoo na baadhi ya miundombinu katika Shule ya Msingi Mwendapole iliyopo Kibaha, mkoani Pwani.


Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo katika kuiunga mkono serikali ili kuhakikisha wanafunzi wanapata miundombinu bora na imara ya kujisomea.


Odemba amefafanua kuwa moja ya malengo ya taasisi yake ni kuhakikisha vyoo vipya zaidi ya 14 vinajengwa, huku vingine vikiendelea kukarabatiwa kwa awamu – jambo litakalohusisha jumla ya vyoo 36 na miundombinu mingine muhimu.


Shule hiyo imekuwa ikikumbwa na changamoto za miundombinu kwa miaka kadhaa sasa, hali inayowaathiri zaidi wanafunzi wa kike kwa kusoma katika mazingira magumu na yasiyo rafiki kwa afya.


“Kutuunga kwako mkono ni muhimu, kwani hakuna mchango mdogo wowote unahitajika kufanikisha hili,” amesema Miriam.


Taasisi ya MOF imejikita katika kumjengea binti wa Kitanzania mazingira wezeshi ya kusoma na kupanga malengo yake ya baadaye, sambamba na kuchangia maboresho katika sekta mbalimbali kama vile urembo, vipaji, sanaa na elimu.


“Sisi tuna upendo, na tunatamani Watanzania wote tuungane kwa pamoja katika kuleta mabadiliko chanya kwa ajili ya jamii yetu,” alisisitiza Miriam.


Miriam amewaomba Watanzania wenye moyo wa kusaidia kuchangia hata kiasi cha Tsh 1,000 au zaidi kupitia:


📱 Simu: 0749 808073  

🔹 Jina litakavyotokea: MIRIAM ODEMBA FOUNDATION

🏦 Benki: NBC  

🔢 Namba ya Akaunti: 011172000038  

👤 Jina:MIRIAM ODEMBA FOUNDATION

Kwa maelezo zaidi au kuchangia mtandaoni, tembelea:[Miriam Odemba Foundation]

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.