DAR ES SALAAM.
Mtaalamu wa majengo (Quantity Surveyor), ambaye pia ni Kada wa CCM QS Joseph Boniface Mhonda, amechukua na kurejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kinondoni.
Hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa ndani ya chama kwa ajili ya kumpata mgombea atakayewakilisha CCM katika uchaguzi mkuu wa 2025
QS Mhonda ameungana na wanachama wengine walioitikia wito wa chama kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa mujibu wa Katiba ya CCM na kanuni zake
Hakuna maoni: