DAR ES SALAAM.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ragi Samwel, amekishukuru chama chake kwa kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao.
Ragi amesema atabaki kuwa mwanachama mtiifu na mwaminifu kwa CCM, huku akisisitiza dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Ukonga kwa kusukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo.
"Nipo tayari kushirikiana na wote waliopata dhamana ya kupeperusha bendera ya chama changu cha CCM. Nitakuwa bega kwa bega na wananchi wa Ukonga kuhakikisha tunaleta maendeleo ya kweli na yanayoonekana," amesema Ragi Samwel.
Hakuna maoni: